Jumamosi 10 Mei 2025 - 19:50

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, asubuhi ya leo katika mkutano wake na maelfu ya wafanyakazi kwenye maadhimisho ya wiki ya kazi na mfanyakazi, alibainisha kuwa utekelezaji wa kaulimbiu ya "Uwekezaji kwa ajili ya uzalishaji" umo chini ya kutolewa kwa umuhimu wa kweli kwa wafanyakazi kama rasilimali muhimu zaidi ya kazi na mojawapo ya nguzo ni uimara na kudumu. Aidha, alisisitiza juu ya mambo ya lazima kama vile kuhakikisha usalama wa ajira na mazingira salama ya kazi kwa wafanyakazi, kuongeza ujuzi wao, na kuwashirikisha katika faida ya uzalishaji. Pia alikumbusha: matumizi ya bidhaa na vitu vya ndani ya Iran vinapaswa kuwa utamaduni katika nchi; bila shaka, sambamba na kueneza utamaduni huo, ubora wa bidhaa za ndani pia unapaswa kuimarishwa.

Ayatullah Khamenei vilevile, kwa kuashiria kuendelea kwa jinai na mauaji ya kikatili dhidi ya watu wa Ghaza na Palestina yanayofanywa na utawala wa Kizayuni kwa msaada wa Marekani na Uingereza, alisisitiza kuwa: Mataifa yanapaswa kusimama dhidi ya utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake, na wasiruhusu masuala yanayohusiana na Palestina yasahaulike.

Kiongozi wa Mapinduzi alihusisha masuala ya kazi na wafanyakazi na hatima ya nchi, na katika kueleza umuhimu wa thamani ya kazi na mfanyakazi alisema: Wafanyakazi wapendwa wanapaswa kujitambua thamani yao, kwani kujipatia riziki ya maisha na mkate wa halali kwa kujiepusha na uporaji, uvivu na kujinufaisha kwa mali ya wengine, pamoja na kutatua mahitaji ya jamii kupitia uzalishaji wa bidhaa na huduma, ni sifa mbili zenye thamani na muhimu za mfanyakazi kwa mtazamo wa kibinadamu ambazo mbele ya Mwenyezi Mungu huhesabiwa kuwa ni mema (hasana).

Ayatullah Khamenei, katika kubainisha thamani ya kazi, alisema: Kazi ni nguzo kuu ya uendeshaji na uimara wa maisha ya mwanadamu, ambayo bila hiyo maisha hukumbwa na kupooza. Hivyo basi, ingawa elimu na mtaji vina nafasi na athari muhimu katika utekelezaji wa kazi, lakini bila mfanyakazi kazi haiwezi kusonga mbele, na ni mfanyakazi ndiye anayeupa uhai mtaji.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha