Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Alireza A'arafi, nyongeza za kongamano la kimataifa la kutimiza miaka mia moja tangu kufufuliwa kwa Hawza ya Qom, huku akitoa shukrani kutokana na chapisho la Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, alisema: Tunamshukuru kwa dhati Kiongozi Mkuu kwa kutoa chapisho la Hawza, na vilevile tunawashukuru Maraaji wakuu wa taqlid ambao kwa uwepo wao na ujumbe wao wa nuru walilitia uzito kongamano hili.
Mkurugenzi wa Hawza alibainisha kuwa: Ujumbe wa kimkakati wa Kiongozi wa Mapinduzi ni nyaraka muhimu zaidi baada ya chpisho la Imam Khomeini (ra), na umefungua upeo mpya mbele ya Hawza.
Ayatollah A'arafi aligusia mgawanyo wa kihistoria wa Hawza na kusema: Hawza ya Qom inaweza kugawanywa kwa ujumla katika vipindi viwili: kabla na baada ya karne ya 14 Hijria. Kwa kila kipindi miongoni mwa hivi viwili, kuna hatua sita za kihistoria zinazoweza kutambuliwa, ambazo zitafafanuliwa kwa upana katika nafasi yake.
Aliongeza: Hivi sasa tuko kwenye mlangoni mwa kuingia katika karne ya kumi na tano Hijria, ambapo hatua ya saba ya maisha ya Hawza imeanza, hatua ambayo ni sura mpya katika historia ya taasisi hii ya kale.
Mkurugenzi wa Hawza nchini Irani aligusia vipengele vikuu vya ujumbe wa Kiongozi Mkuu na kusema: Kiongozi wa Mpinduzi katika ujumbe wake wa kihistoria amebainisha nguzo tano kuu kwa ajili ya Hawza, ambapo kipengele cha mwisho ni ujumbe wa kistaarabu wa Hawza na mtazamo wa kuelekea upeo wa juu wa ustaarabu. Ujumbe huu wa hali ya juu utakuwa mwongozo wetu katika njia ya mageuzi na maendeleo ya Hawza.
Ayatollah A'arafi alitangaza hatua za utekelezaji wa chapisho la Kiongozi Mkuu na kusema: Uhakiki na uchambuzi wa mkataba wa Hawza uliotolewa na Kiongozi Mkuu umeanza, na hivi karibuni baraza litaundwa kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wake. Masuala ya kimkakati ya nyaraka hii yamepangwa katika mfumo maalumu.
Alisisitiza: Pamoja na kukamilika kwa mpango wa kwanza wa miaka mitano, sasa tupo katika hatua ya kuandaa mpango wa pili wa Hawza, ambao ndani yake, miongozo yote ya Kiongozi Mkuu na mahitaji yake ya msingi yatawekwa.
Mkurugenzi wa Hawza nchini Irani alizungumzia mipango ya baadaye na kusema: Miradi muhimu ya mageuzi ya Hawza itasomwa upya na kutekelezwa kwa mujibu wa misingi hii. Leo, sambamba na mji wa Qom, katika vituo vya kielimu vya Hawza ndani na nje ya nchi, maelfu ya watu wamesikia ujumbe huu na roho mpya imepulizwa katika mwili wa Hawza.
Ayatollah A'arafi alihitimisha kwa kusema: Tunamuomba Mwenyezi Mungu Muweza msaada katika njia hii, na tunatarajia kwa baraka za Maimamu Watoharifu (a.s) na juhudi za wanafunzi na walimu, tuwe mashahidi kwenye utekelezaji wa malengo haya makuu. Nawashukuru kwa dhati Maraaja wakubwa, maulamaa, walimu na vyombo vya habari, hasa vile vinavyohusiana na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi.
Maoni yako