Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Tuzo hiyo ilikabidhiwa, tarehe 17 Desemba 2025, katika hafla rasmi iliyofanyika nchini Iran, huku wakishiriki wa viongozi mbali mbali wa kidini, kisiasa, kijamii na wawakilishi wa taasisi mbalimbali.
Kwa mujibu wa waandaaji wa tuzo hiyo, Sheikh Zakzaky anatambuliwa kama mmoja wa viongozi mashuhuri walioweka maisha yao wakfu katika kupigania haki, uadilifu wa kijamii na mshikamano wa Ummah, kwa kuzingatia misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu yaliyoasisiwa na Imam Khomeini (ra). Tuzo hii ni ishara ya heshima na kuthaminiwa kimataifa, kutokana na mchango wake wa muda mrefu katika kuhamasisha uamsho wa Kiislamu na kusimama imara upande wa waliodhulumiwa.







Maoni yako