Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, sambamba na kuongezeka kwa mabadiliko ya kikanda, “Mkutano wa sita wa kielimu wa kila mwaka wa Jumuiya ya Kiarabu ya elimu ya Siasa” wenye anuani “Harakati za ukombozi na uhuru katika dunia ya tatu na mafunzo yaliyopatikana kutoka muqawama wa Palestina”, ulianza kazi zake chini ya usimamizi wa Chuo Kikuu cha Lebanon mjini Beirut. Mkutano huu, ulioshuhudiwa na idadi kubwa ya watu wa kisiasa, vyama na utamaduni, ulikuwa jukwaa la kusisitiza upya haki ya kupinga, uthabiti wa misimamo, na ulazima wa kutumia nyenzo zote dhidi ya mipango ya kikanda ya adui. Watoa hotuba kutoka pande mbalimbali walisisitiza umoja wa Wapalestina na kusimama imara dhidi ya mashinikizo ya kimataifa.
Kundi la Bunge la “Uaminifu kwa muqawama”
Katika mwendelezo wa mkutano, Ihab Hamadeh, mjumbe wa kundi la bunge la “Uaminifu kwa muqawama” na mwakilishi wa Sheikh Na‘im Qasim, Katibu Mkuu wa Hizbullah, aliisifu nafasi ya kitamaduni ya Jumuiya ya Kiarabu ya Sayansi ya Siasa na akasisitiza ulazima wa kutumia nyenzo zote kukabiliana na adui.
Alionya kuhusu hatari ya mradi wa “Israel Kubwa” na tamaa zake katika eneo, na akazihimiza nchi za Kiarabu na mataifa huru kufanya tathmini upya ya “ramani ya bluu” iliyowasilishwa na waziri mkuu wa utawala wa kikoloni, Benjamin Netanyahu.
Harakati ya Amal
Kwa upande mwingine, Zaki Juma‘a, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Amal, alisisitiza kuwa mashinikizo yanayowekwa kwa Lebanon kupitia kampeni za vyombo vya habari na kisiasa pamoja na misafara ya ujumbe wa kisiasa, yataishia kuongeza tu azma na uthabiti wa msimamo wa Lebanon.
Aliongeza: Hakuna shinikizo lolote kati ya haya linaloweza kuwazuia watu wa Lebanon na upinzani kutekeleza majukumu yao kuhusu suala la Palestina.
Juma‘a pia aliziheshimu roho za mashahidi wa Lebanon, Palestina na nchi zote za mhimili wa upinzani.
Harakati ya Hamas
Kwa upande wake, Ahmad ‘Abd al-Hadi, mwakilishi wa Harakati ya Hamas nchini Lebanon, alisisitiza kushikamana na haki ya kupambana dhidi ya mkoloni huku akisema: Makundi ya Kipalestina hayataweka chini silaha zao kamwe; kwa sababu silaha hizo ndizo roho na heshima yao.
Alisisitiza uthabiti wa msimamo na umoja wa safu kwa ajili ya kuhudumia watu wa Palestina, na akaashiria kuwa: Makundi yote ya Kipalestina yatakuwa na unyumbufu unaohitajika kwa ajili ya kuvuka kwenda hatua ya pili ya makubaliano, kwa namna itakayohudumia maslahi ya watu wa Ghaza na kupunguza mateso yao.
Wakati huohuo, ‘Abd al-Hadi alisisitiza ulazima wa kuweka shinikizo kwa adui ili atekeleze vipengele vya makubaliano.
Harakati ya Jihad ya Kiislamu
Ihsan ‘Attaya, mwakilishi wa Harakati ya Jihad ya Kiislamu nchini Lebanon, katika hotuba yake alitoa wito wa kushikamana na umoja wa Wapalestina mbele ya mkoloni, akisisitiza: Migawanyiko kati ya ya Wapalestina daima imekuwa kwa faida ya adui, ilhali umoja na msimamo wa pamoja ni chanzo cha nguvu ya upinzani.
Kituo cha Tafiti za Umoja wa Kiarabu
Dkt. Jamal Wakim, mwakilishi wa Kituo cha Tafiti za Umoja wa Kiarabu, katika hotuba yake alisisitiza umuhimu wa mafanikio chanya yaliyopatikana kutokana na harakati za ukombozi katika eneo, na akakumbusha nafasi yake katika kuimarisha roho ya muqawama na kukabiliana na ukoloni.
Georges Abdallah
Kwa upande wake, Georges Abdallah, huku akisisitiza kuwa; Lebanon leo iko mstari wa mbele wa nchi za muqawama sambamba na Palestina, aliongeza: Njama za kimataifa dhidi ya eneo ni ushahidi kwamba tunatembea katika njia sahihi; njia ya muqawama na mapambano dhidi ya ubeberu duniani.
Ghassan Ben Jeddou mwakilishi wa Rony Alfa
Rony Alfa, kwa niaba ya Ghassan Ben Jeddou, rais wa mtandao wa vyombo vya habari wa al-Mayadeen, alitoa hotuba na kusisitiza umuhimu wa silaha ya akili na neno, katika kufichua ukweli, kuangaza njia sahihi, na kuhifadhi ushahidi wa uhalifu wa adui.
Kuendelea mkutano huo
Mkutano huu utaendelea kwa muda wa siku mbili, na utajumuisha mfululizo wa shughuli na vikao maalumu vinavyohusiana na muqawama na harakati za ukombozi.
Maoni yako