Alhamisi 18 Desemba 2025 - 18:59
Taasisi ya Kawthar Yafanya Hafla ya “Siku ya Kimataifa ya Wanawake Wakiislamu” Nchini Uturuki

Hawza/ Kituo cha Kitamaduni cha Kawthar, kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa Bibi Fatima Zahra (a.s.) na Siku ya Kimataifa ya Wanawake Wakiislamu, kiliandaa hafla ya kiroho iliyowakutanisha wapenzi wa Ahlul-Bayt (a.s.).

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, hafla hii iliandaliwa kwa juhudi za tawi la wanawake la Taasisi ya Kawthar katika Msikiti wa Ahlul-Bayt Kawthar, na ilipokelewa kwa ushiriki mkubwa wa watu. Katika mwendelezo wa programu, kulisisitizwa uhusiano wa Sura ya Kawthar na haiba ya Bibi Fatima Zahra (a.s.), pamoja na nafasi yake ya kuhamasisha katika maisha.

Washiriki waliopopokelewa, mwanzoni walikaribishwa na tawi la wanawake la Kawthar, na walipewa zawadi zenye mada ya Palestina kama ishara ya mshikamano na watu wa ardhi hiyo.

Baadaye, Belgin Güneş, kwa niaba ya tawi la wanawake la Kawthar, aliwakaribisha waliohudhuria, akawapongeza kwa Siku ya Kimataifa ya Wanawake Wakiislamu, na kusisitiza umuhimu wa kuiga vitendo, mwenendo na maisha ya Bibi Fatima Zahra (a.s.) katika nyanja zote za maisha.

Hafla hii iliambatana na usomaji wa mashairi, hotuba kuhusiana na maisha na mwenendo wa Bibi Zahra (a.s.), pamoja nautekelezaji wa dua, pia kulikuwa na utoaji wa zawadi maalumu kwa washiriki waliobeba majina ya Fatima na Zahra. Mwishoni, waandaaji walitoa shukrani kwa wageni kwa kuhudhuria, na wakasisitiza kuendelea kuandaa programu kama hizi katika mazingira yaliyojaa imani, umoja na mapenzi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha