Jumatano 4 Februari 2026 - 19:17
Sheikh Mkuu wa TIC Ashiriki Upandishaji wa Bendera ya Imam Mahdi (a.s) Bilal Comprehensive School

Hawza/ Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Maulana Sheikh Hemedi Jalala, ameshiriki katika zoezi la upandishaji wa Bendera ya Imam Mahdi (a.s), lililofanyika katika Shule ya Bilal Comprehensive School, tukio lililohudhuriwa na viongozi wa dini, masheikh pamoja na waumini kutoka taasisi mbalimbali.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Akizungumza katika hafla hiyo, Sheikh Jalala alisisitiza nafasi ya Imam Mahdi (a.s) katika historia na mustakabali wa wanadamu, akieleza kuwa Imam Mahdi (a.s) si muokozi wa Waislamu pekee, bali ni muokozi wa umma wa mwanadamu wote duniani, bila kujali dini, madhehebu wala tofauti za kikabila.

“Imam Mahdi (a.s) ni muokozi wa Ummah na wanadamu wote. Imani ya kuwepo kwa muokozi wa mwisho ni imani inayoshirikishwa na watu wengi duniani,” alisema Sheikh Jalala.

Ahadi Tano kwa Imam wa Zama (a.s)

Katika hotuba yake, Sheikh Jalala alieleza kuwa Waislamu na wafuasi wa Ahlul Bayt (a.s) wanatoa ahadi tano muhimu kwa Imam Mahdi (a.s), ambazo wataendelea kuzishikilia hadi siku ya kudhihiri kwake.

Mosi, Kushikamana na Umoja miongoni mwa Wafuasi wa Ahlul Bayt (a.s)

Sheikh Jalala alieleza kuwa umoja miongoni mwa wafuasi wa Ahlul Bayt (a.s) ni msingi wenye nguvu na maendeleo katika wafuasi hao. Alionya kuwa migogoro ya ndani, chuki na mifarakano miongoni mwao inaweza kudhoofisha dhamira ya haki na kusababisha matatizo makubwa katika jamii. Alisisitiza kuwa, kila mfuasi anatakiwa kujenga mshikamano, kusameheana, kusaidiana na kuweka mbele maslahi ya dini na umma badala ya maslahi binafsi.

Pili,  Kudumisha Umoja miingoni mwa Waislamu Wote Nchini Tanzania

Ahadi ya pili ni kudumisha umoja miongoni mwa Waislamu wote nchini Tanzania bila kujali tofauti za kimadhehebu. Kiongozi wa Mashia nchini Tanzania alibainisha kuwa; Uislamu ni dini ya umoja, na kwamba migawanyiko ya kimadhehebu haipaswi kuwa chanzo cha kuleta chuki au migogoro. Alitoa wito kwa Waislamu kushirikiana katika masuala ya kheri, maendeleo ya kijamii, kulinda heshima ya Uislamu na kusimama pamoja dhidi ya maadui wa amani na mshikamano.

Tatu, Umoja wa Kitaifa kwa Watanzania Wote

Katika ahadi ya tatu, Sheikh Jalala alisema kuwa wafuasi wa Ahlul Bayt (a.s) wana wajibu wa kulinda na kuimarisha umoja wa kitaifa kwa Watanzania wote bila kujali tofauti za kidini, kikabila au kisiasa. Alisisitiza kuwa; Tanzania ni taifa linalojengwa juu ya misingi ya amani na mshikamano, na kwamba kudumisha umoja huo ni sehemu ya kutekeleza maadili ya Kiislamu na kusubiri kwa vitendo kudhihiri kwa Imam Mahdi (a.s).

Nne, Kuvumiliana na Kuishi kwa Amani

Ahadi ya nne ni kuvumiliana, kuishi pamoja na kwa amani, kuepuka vurugu na kujenga mapenzi miongoni mwa watu. Sheikh Jalala alieleza kuwa; subira, heshima na mazungumzo ya busara ni silaha muhimu katika kukabiliana na tofauti za maoni ndani ya jamii. Alisisitiza kuwa; jamii inayovumiliana ndiyo jamii inayokaribia zaidi maadili ya haki na uadilifu anaokuja kuusimamisha Imam Mahdi (a.s).

Tano, Kudumisha Amani, Utulivu na Uadilifu

Ahadi ya tano ni kudumisha amani, utulivu na uadilifu katika jamii. Kiongozi huyo wa Mashia nchini Tanzania alisema kuwa; kusimamia haki, kupinga dhulma na kuishi kwa uadilifu ni maandalizi ya kweli ya kumpokea Imam wa Zama (a.s). Aliongeza kuwa; amani ya kweli haiji kwa maneno pekee, bali kwa vitendo vya haki, uadilifu na kuwajali wanyonge katika jamii.

Mwisho wa hafla hiyo, Sheikh Hemed Jalala aliwashukuru waumini wote walioshiriki katika tukio hilo, pamoja na viongozi na masheikh wa Bilal Muslim Mission kwa mchango wao katika kufanikisha zoezi hilo.

Aidha, aliwaongoza waumini katika dua ya pamoja kumuomba Mwenyezi Mungu (swt) aharakishe kudhihiri kwa Imam wa Zama (a.s) na kudumisha amani na mshikamano katika jamii.

Sheikh Mkuu wa TIC Ashiriki Upandishaji wa Bendera ya Imam Mahdi (a.s) Bilal Comprehensive School

Sheikh Mkuu wa TIC Ashiriki Upandishaji wa Bendera ya Imam Mahdi (a.s) Bilal Comprehensive School

Sheikh Mkuu wa TIC Ashiriki Upandishaji wa Bendera ya Imam Mahdi (a.s) Bilal Comprehensive School

Sheikh Mkuu wa TIC Ashiriki Upandishaji wa Bendera ya Imam Mahdi (a.s) Bilal Comprehensive School

Sheikh Mkuu wa TIC Ashiriki Upandishaji wa Bendera ya Imam Mahdi (a.s) Bilal Comprehensive School

Sheikh Mkuu wa TIC Ashiriki Upandishaji wa Bendera ya Imam Mahdi (a.s) Bilal Comprehensive School

Sheikh Mkuu wa TIC Ashiriki Upandishaji wa Bendera ya Imam Mahdi (a.s) Bilal Comprehensive School

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha