Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, tukio hili la kitamaduni la “Kuutafiti Uislamu”, ambalo linatarajiwa kufanyika katikati ya mwezi Agosti katika maktaba hiyo, litawakutanisha wananchi wote na familia zao bila malipo, ili wapate fursa ya kutumia vitabu vinavyohusu masuala mbalimbali ya Kiislamu.
Hata hivyo, kwa masikitiko, baadhi ya watu wanaopinga kuenea kwa mafundisho sahihi ya Kiislamu nchini Uingereza wamewasilisha malalamiko na ukosoaji dhidi ya programu hiyo ya kitamaduni. Wamedai kuwa mpango huo unaifanya maktaba kuwa chombo cha kutangaza fikra maalumu, ilhali maktaba inapaswa kuwa taasisi isiyoegemea upande wowote.
Mmoja wa viongozi wa waandaaji wa tukio hilo alijibu ukosoaji huo kwa kusema: "Kinyume chake, ikiwa tutatoa ufafanuzi sahihi na wa wazi kuhusu Uislamu, basi hatua hii ni maendeleo muhimu katika kujenga uelewa sahihi wa kimawazo."
Kikundi kinachoandaa tukio hilo kilitangaza kuwa maonyesho hayo yatafanyika katika vituo vya kijamii, maktaba na maeneo mengine ya umma. Maonesho hayo ya Kiislamu yataandaliwa kwa mtindo wa makumbusho, yakiwapa wageni fursa ya kujifunza kuhusu imani, historia, utamaduni na maisha ya kila siku ya Waislamu kupitia mazungumzo ya wazi na maonesho shirikishi.
Chanzo: Manchester Evening News
Maoni yako