Jumapili 13 Septemba 2026 - 00:33
TIC Yafika Zanzibar; Sheikh Jalala Aongoza Ujumbe wa Pole kwa Rais Samia, Kufuatia Msiba wa Mumewe

Hawzah/ Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge, siku ya jana amefanya ziara ya Zanzibar kuelekea Kizimkazi kwa lengo la kutoa mkono wa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kufuatia msiba wa mumewe, Bwana Hafidh Amer Hassan.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Bwana Hafidh Amer Hassan alifariki dunia tarehe 7 Septemba 2026 huko Zanzibar, alipokuwa akipatiwa matibabu hospitalini, msiba huo umeleta huzuni kwa familia, ndugu, jamaa na Watanzania kwa ujumla, huku viongozi na watu mbalimbali wakifika kutoa pole na kushiriki katika kuifariji familia katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Katika ziara hiyo, msafara wa Sheikh Jalala ulipata pia fursa ya kupita katika Ofisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyopo Kisiwandui, Zanzibar, ambapo ulisaini katika Daftari la Wageni kabla ya kuendelea na safari kuelekea Kizimkazi.

Ziara hiyo imeelezwa kuwa ni sehemu ya kuendeleza utamaduni wa Kiislamu na kijamii wa kutoa pole, kuifariji familia iliyopatwa na msiba na kusimama pamoja katika nyakati za huzuni.

Sheikh Jalala katika ziara hiyo, ameongozana na Makamu wake, Samahat Sheikh Mohamed Abdi; Makamu Mwenyekiti, Abdulkarim Shamte; Katibu Nyello; pamoja na Naibu Katibu wa Wanawake wa TIC, Kijoli Jumaa Wema. Msafara huo umeongozwa pia na mwenyeji wao, Hesmen Haloo, katika safari yao kuelekea Kizimkazi.

TIC Yafika Zanzibar; Sheikh Jalala Aongoza Ujumbe wa Pole kwa Rais Samia Kufuatia Msiba wa Mumewe

TIC Yafika Zanzibar; Sheikh Jalala Aongoza Ujumbe wa Pole kwa Rais Samia Kufuatia Msiba wa Mumewe

TIC Yafika Zanzibar; Sheikh Jalala Aongoza Ujumbe wa Pole kwa Rais Samia Kufuatia Msiba wa Mumewe

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha