Alhamisi 12 Novemba 2026 - 10:30
Sheikh Mkuu wa Shia Tanzania Ahudhuria Maulid ya Mabohora Dar es Salaam, Rais Mwinyi Awa Mgeni Rasmi

Hawza/ Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge, ameshiriki katika hafla kubwa ya Maulid ya Mabohora iliyofanyika jana, jijini Dar es Salaam, katika msikiti wa waumini wa madhehebu hayo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hafla hiyo ya kipekee, iliyokusanya viongozi mbalimbali wa Kidini na kisiasa pamoja na wageni mashuhuri, imefanyika katika mazingira ya kuimarisha mshikamano, maelewano na uhusiano mwema baina ya viongozi wa dini na jamii kwa ujumla.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ambaye aliongozana na viongozi wengine mbalimbali walioshiriki katika maadhimisho hayo.

Ushiriki wa Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge, katika hafla hiyo unaendelea kuonesha umuhimu wa mawasiliano na ushirikiano baina ya viongozi wa madhehebu na taasisi mbalimbali za kidini katika kuimarisha umoja, upendo na kuishi kwa amani miongoni mwa jamii.

Maulid ya Mabohora ni miongoni mwa matukio yanayowakutanisha waumini na viongozi mbalimbali, ikiwa pia ni fursa ya kudumisha uhusiano wa kijamii na kuendeleza misingi ya kuheshimiana na mshikamano.

Sheikh Mkuu wa Shia Tanzania Ahudhuria Maulid ya Mabohora Dar es Salaam, Rais Mwinyi Awa Mgeni Rasmi

Sheikh Mkuu wa Shia Tanzania Ahudhuria Maulid ya Mabohora Dar es Salaam, Rais Mwinyi Awa Mgeni Rasmi

Sheikh Mkuu wa Shia Tanzania Ahudhuria Maulid ya Mabohora Dar es Salaam, Rais Mwinyi Awa Mgeni Rasmi

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha