تیتر سه زیرسرویس
-
Hadithi ya leo:
Kuwa hivi katika maingiliano na watu
Ingilianeni na watu kwa namna ambayo mkifa wakulilieni, na mkiwa hai (na ikawa hawajakuoneni kwa muda) wawe na shauku ya kukuoneni.
-
Hadithi ya leo:
Lipe uzito suala la haki za watu
Mwenye kula mali ya nduguye kwa dhulma na asimrudishie mwenyewe, basi chakula chake Siku ya Kiyama ni miali ya moto.
-
-
Hadithi ya leo:
Sema haki, kwani kuokoka kwako kuko katika hilo
Mche (muogope) Mwenyezi Mungu na sema haki hata kama utaangamia, kwani (kwa hakika) kuokoka kwako kuko katika hilo. Mche Mwenyezi Mungu na acha batili hata kama kuokoka kwako kuko katika hilo,…
-
Hadithi ya leo:
Usipuuze sauti ya wengine ya kuomba msaada
Mwenye kusikia sauti ya mwenye kuomba msaada na asiende kumsaidia, huyo sio Muislamu.
-
Hadithi ya leo:
Katu usifanye khiana katika amana
Mcheni Mwenyezi Mungu na rudisheni amana kwa yule aliyekuaminini.
-
Hadithi ya leo:
Ni wajibu kwako kuchunga haki za kila mtu (awe Muislamu au sio Muislamu)
Kuna makundi mawili ya watu: Ama ni ndugu yako katika dini, au anayefanana na wewe katika uumbaji; kwa hali yoyote, unapaswa kuheshimu haki zao.
-
Hadithi ya leo:
Chunga (mazingira) asili
Itakapowadia Siku ya Kiyama na mmoja wenu akawa ana mche mkononi mwake, akiweza kuupanda kabla ya kusimama Kiyama, basi aupande.
-
Hadithi ya leo:
Chunga haki za wanyama
Kila unapowakabidhi wanyama kwa mtu mwaminifu, muagizie asitengananishe kati ya ngamia na mtoto wake, na asikamue maziwa yake kiasi cha kumdhuru mtoto... .
-
Hadithi ya leo:
Kuwa hivi kwa watu
Kuwa mlaini kwa watu, kuwa na maneno mazuri na kutana na ndugu yako kwa bashasha na tabasamu.
-
Hadithi ya leo:
Jipambe kwa tabia njema
Tabia njema ni; Kumsamehe aliyekudhulumu, kuunga udugu aliyekukatia (udugu), kumpa aliyekunyima na kusema haki hata kama ni kwa madhara yako.
-
Hadithi ya leo:
Kuwa mtu wa utani (mzaha), lakini chunga mpaka wake
Mwenyezi Mungu anampenda afanyae mzaha katika mkusanyiko, kwa sharti asitukane na kutoa maneno machafu.
-
Hadithi ya leo:
Kuwa hivi katika biashara
Yeyote anayefanya biashara (anauza na kununua) lazima aepuke vitu vitano, kinyume na hivyo asinunue au kuuza kabisa: Riba, kuapa, kuficha ubovu (wa bidhaa), kusifu bidhaa anazouza, na kukashifu…
-
Hadithi ya leo:
Usiache wajibu hizi mbili kubwa za Mwenyezi Mungu
Kwa hakika kuamrisha mema na kukataza maovu ni faradhi mbili kubwa, kwazo faradhi husimamishwa.
-
Hadithi ya leo:
Uombezi wa mwanamke mbele ya Mwenyezi Mungu
Hakuna uombezi wa mwanamke mbele ya Mwenyezi Mungu wenye kuokoa zaidi kama radhi ya mumewe. (mumewe kuwa radhi naye)
-
Hadithi ya leo:
Lipe uzito suala la heshima na ridhaa ya mwenza
Hakika aliye mbora zaidi miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule ambaye anamheshimu zaidi mwenza wake.
-
Hadithi ya leo:
Weka mambo yako katika mkondo wa haki
Hakuacha haki mwenye izza (heshima) isipokuwa alidhalilishwa, na dhalili hakuchukua haki isipokuwa alipata izza (heshima).
-
Hadithi ya leo:
Daima kuwa mtu huru
Usiwe mtumwa wa mwingine, ilihali Mwenyezi Mungu amekuumba ukiwa huru.
-
Hadithi ya leo:
Jiepushe na talaka
Oeni wala msitaliki, kwani hakika talaka inatikisha arshi ya Mwenyezi Mungu.
-
Hadithi ya leo:
Ifundishe familia yako maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu
Katika kauli yake Mwenyezi Mungu alotukuka utajo wake" Jiokoeni nafsi zenu na familia zenu na moto".