Jumatano 22 Julai 2026 - 13:10
Hadithi ya Leo | Katazo la Kuwadharau Watu na Kuwadunisha

Hawza/ Mtume Mtukufu (saww) katika riwaya amekataza kuwadharau na kuwadunisha.

Shirika la Habari la Hawza limechapisha riwaya ifuatayo kutoka katika kitabu cha Bihar al-Anwar:

لَا يَزْرَأَنَّ أَحَدُكُمْ بِأَحَدٍ مِنْ خَلْقِ اللَّهِ فَإِنَّهُ لَا يَدْرِي أَيُّهُمْ وَلِيُّ اللَّهِ

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) amesema:

Asidharau mmoja wenu kumdharau mwengine au kumwona duni yeyote miongoni mwa viumbe wa Mwenyezi Mungu; kwani hajui ni nani miongoni mwao ambaye ni kipenzi wa Mwenyezi Mungu.

Chanzo: Bihar al-Anwar, Juz. 72, uk. 147.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha