Jumatatu 7 Septemba 2026 - 11:15
Iraq Inahitaji Serikali Itakayowaokoa Wananchi na Kulinda Utawala wa Nchi

Hawza/ Ayatullah Sayyid Yasin Al-Mousawi, Imam wa Ijumaa wa Baghdad, amekosoa sera za kiuchumi na utendaji wa kisiasa wa baadhi ya viongozi, huku akisisitiza umuhimu wa kuundwa serikali ya wananchi, yenye uadilifu na iliyo huru dhidi ya uingiliaji wa mataifa ya kigeni.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Yasin Al-Mousawi, Imam wa Ijumaa wa Baghdad na mmoja wa walimu mashuhuri wa Hawza ya Najaf Ashraf, katika khutba yake ya kisiasa iliyotolewa tarehe 4 Septemba 2026 (13 Shahrivar 1405), alisisitiza kwamba, Iraq kwa sasa inakabiliwa na tatizo la uwazi na kutokuwepo uelewa wa wazi kuhusu mpango wa serikali mpya.

Alisema: “Ujenzi wa serikali haupaswi kuwa lengo lenyewe, bali ni lazima uambatane na utekelezaji wa uadilifu; kwa sababu serikali inayoendeshwa bila uadilifu hupoteza lengo na falsafa ya uwepo wake.” Kisha, akieleza kwamba athari za sera za serikali zinaonekana wazi katika uwanja wa uchumi, alikosoa kuendelea kwa baadhi ya sera na hatua zilizochukuliwa, akisema kuwa hatua hizo zimeongeza zaidi mzigo kwa wananchi na kuwalazimisha kubeba gharama za hasara ambazo serikali imezipata katika miaka iliyopita.

Ayatullah Al-Mousawi pia alionya kuhusu madhara ya mkwamo wa kiuchumi kwenye jamii, akisema: “Kupungua uwezo wa wananchi wa kununua kumesababisha kudorora kwa shughuli za kiuchumi na kufungwa sehemu kubwa za masoko. Bidhaa na huduma ambazo miaka michache iliyopita zilihesabiwa kuwa mahitaji ya kawaida au hata bidhaa za anasa, leo zimekuwa hazipatikani kwa wananchi wa Iraq.”

Aliongeza: “Kuendelea kwa umaskini na matatizo ya kimaisha kumeacha athari zake pia katika maisha ya kifamilia na kijamii, na kusababisha kuongezeka matatizo na madhara ya kijamii ndani ya jamii.”

Katika uwanja wa kisiasa, Ayatullah Al-Mousawi alikosoa utendaji wa baadhi ya wanasiasa, akisema kuwa baadhi yao wamezoea mfumo ambao wanapokabiliwa na migogoro na shinikizo, hurudi nyuma na kuendana na hali iliyopo; lakini baada ya mgogoro huo kumalizika, hurudia tena mtazamo na mwenendo wao wa zamani.

Akirejelea wito uliowahi kutolewa na Marja'iyyah Kuu ya Kidini wa kubadili mfumo huo wa kisiasa, alisisitiza umuhimu wa kuwachagua viongozi na watu wapya ambao wananchi hawajawahi kuwa na uzoefu hasi na usioridhisha kuhusu utendaji wao hapo awali.

Imam wa Ijumaa wa Baghdad alisisitiza: “Taifa lenye uelewa halipaswi kunyamaza tu, bali linapaswa kusema, kudai haki zake na kuwawajibisha viongozi.”

Aidha, alitoa wito wa juhudi za pamoja, chini ya uongozi wa Marja'iyyah Kuu ya Kidini, za kujenga uongozi wa kisiasa wa siku zijazo ambao utakuwa na elimu, uadilifu na uwezo wa kuiongoza nchi pamoja na kurekebisha hali iliyopo.

Ayatullah Al-Mousawi pia alikosoa kwa ukali kile alichokiita kuwa ni utegemezi wa baadhi ya wanasiasa kwa Marekani, huku akisisitiza kwamba maamuzi kuhusu masuala yanayohusiana na mamlaka ya Iraq, ikiwemo suala la kuwa na silaha chini ya mamlaka ya serikali pekee, inapaswa kuwa suala la ndani na la Kiiraq, na haipaswi kuathiriwa na maagizo au shinikizo kutoka nje.

Alionya pia kuhusu madhara yanayoweza kusababishwa na kukabidhi silaha, huku akiuliza swali kwamba: “Ni nani anayeamua ‘maslahi ya Iraq’?”

Katika suala hilo, alieleza wasiwasi wake kwamba hatua kama hiyo inaweza hatimaye kusababisha shinikizo dhidi ya makamanda wa Muqawama na wapiganaji wa jihadi, na kwamba athari zake zinaweza kuendelea hadi kufikia kubadilishwa kwa utambulisho, muundo wa uongozi, mwelekeo na utamaduni wa kidini wa Al-Hashd Al-Sha'abi.

Imam wa Ijumaa wa Baghdad alihitimisha khutba yake kwa kusisitiza: “Tatizo kuu la Iraq si silaha wala mafuta, bali ni ‘enzi na uhuru wa maamuzi ya kisiasa’.” Alitoa wito wa kuundwa serikali ambayo kwa hakika itakuwa serikali ya wananchi, itakayojitahidi kuwaokoa wananchi na kutekeleza uadilifu, na ambayo itakuwa mbali na utegemezi wa madola ya kigeni.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha