Jumatano 26 Agosti 2026 - 06:00
Bendera ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) Yapandishwa Kigogo: Sheikh Jalala Atoa Wito wa Upendo, Amani na Mshikamano

Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge, ameongoza zoezi la upandishaji wa Bendera ya Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w), katika hafla iliyofanyika katika Msikiti wa Ghadiir, Kigogo Post, jijini Dar es Salaam, kwenye Makao Makuu ya Jumuiya hiyo. Zoezi hilo limefanyika ikiwa ni sehemu ya ufunguzi wa maadhimisho na kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambaye ni kiongozi na mfano bora wa maisha kwa Waislamu duniani.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, katika hafla hiyo, Sheikh Jalala ametoa salamu za Maulid kwa Waislamu wote, huku akisisitiza umuhimu wa waumini kutumia fursa ya maadhimisho hayo kutafakari na kuhuisha mafundisho ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika maisha yao ya kila siku. Amesema Maulid si tukio la kusherehekea pekee, bali ni wakati muhimu wa kurejea katika mwenendo, maadili na mafundisho ya Mtume (s.a.w.w).

Sheikh Jalala amewataka Waislamu nchini Tanzania kuishi kwa upendo, amani na mshikamano, huku akisisitiza kuwa umoja na kuheshimiana ni miongoni mwa misingi muhimu iliyofundishwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w). Ameeleza kuwa jamii inapojengwa juu ya misingi hiyo, huimarisha mahusiano baina ya watu na kuweka mazingira ya amani na maendeleo.

Aidha, Sheikh Mkuu huyo amesisitiza kwamba mafundisho ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) hayapaswi kuishia ndani ya jamii ya Waislamu pekee, bali yanapaswa kuonekana pia katika namna Waislamu wanavyowatendea na kuishi pamoja na watu wasiokuwa Waislamu. Amesema Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambaye ni Kiumbe Bora wa ulimwenguni, alifundisha kuheshimu utu wa mwanadamu, kuishi kwa amani, kuhurumiana na kujenga mahusiano mema na watu wote.

Hafla hiyo ya upandishaji wa Bendera ya Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika Masjid Ghadiir imekuwa pia sehemu ya kuwakumbusha Waislamu umuhimu wa kuifanya misingi ya Maulid kuwa sehemu ya maisha yao. Ujumbe wa Sheikh Jalala umebeba wito wa kuendeleza upendo, mshikamano, amani na kuheshimiana, ili jamii ya Tanzania iendelee kuwa mfano wa watu wanaoishi pamoja kwa umoja na maelewano, sambamba na kuenzi mafundisho na mwenendo wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Bendera ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) Yapandishwa Kigogo: Sheikh Jalala Atoa Wito wa Upendo, Amani na Mshikamano

Bendera ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) Yapandishwa Kigogo: Sheikh Jalala Atoa Wito wa Upendo, Amani na Mshikamano

Bendera ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) Yapandishwa Kigogo: Sheikh Jalala Atoa Wito wa Upendo, Amani na Mshikamano

Bendera ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) Yapandishwa Kigogo: Sheikh Jalala Atoa Wito wa Upendo, Amani na Mshikamano

Bendera ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) Yapandishwa Kigogo: Sheikh Jalala Atoa Wito wa Upendo, Amani na Mshikamano

Bendera ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) Yapandishwa Kigogo: Sheikh Jalala Atoa Wito wa Upendo, Amani na Mshikamano

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha