Jumatano 26 Agosti 2026 - 07:00
Baraza la Maulidi Lawaunganisha Viongozi wa Dini: Waziri Mkuu Atoa Wito wa Umoja, Upendo na Mshikamano

Hawzah/ Baraza la Maulidi limefanyika leo Jumanne likiongozwa na Mufti wa Tanzania, huku likiwakutanisha Masheikh na viongozi mbalimbali wa dini katika hafla iliyolenga kuadhimisha mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kuhuisha mafundisho yake katika jamii. Hafla hiyo imekuwa pia fursa ya viongozi wa dini kukutana pamoja na kusisitiza umuhimu wa kudumisha misingi ya amani na mshikamano nchini.

Kwa mujibubu Shirika la Habari la Hawza, miongoni mwa viongozi walioshiriki katika Baraza hilo ni Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindege, aliyewakilisha rasmi Jumuiya ya Shia Tanzania. Ushiriki wake umeendelea kuonesha umuhimu wa ushirikiano na maelewano baina ya viongozi na jumuiya mbalimbali za Kiislamu katika kuimarisha umoja wa Waislamu na jamii kwa ujumla.

Mgeni rasmi katika Baraza hilo alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, aliyemwakilisha Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Ujumbe wa serikali katika hafla hiyo umeakisi umuhimu unaotolewa katika kuendeleza mawasiliano, ushirikiano na mahusiano mema kati ya serikali na viongozi wa dini katika masuala yanayolenga ustawi wa jamii.

Katika hotuba yake, Waziri Mkuu amewahimiza wananchi kudumisha umoja na mshikamano, huku akisisitiza pia umuhimu wa kuishi kwa upendo na kuheshimiana. Ameeleza kuwa misingi hiyo ni muhimu katika kuendelea kulinda amani na utulivu wa Tanzania, pamoja na kuimarisha mahusiano mema miongoni mwa wananchi.

Baraza la Maulidi Lawaunganisha Viongozi wa Dini: Waziri Mkuu Atoa Wito wa Umoja, Upendo na Mshikamano

Baraza la Maulidi Lawaunganisha Viongozi wa Dini: Waziri Mkuu Atoa Wito wa Umoja, Upendo na Mshikamano

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha