Jumanne 25 Agosti 2026 - 23:55
Jumuiya ya Madaktari ni Hazina Adimu ya Elimu, Ujuzi na Maadili ya Kitaaluma

Hawzah/ Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran amesema kuwa; jumuiya ya wasomi wa udaktari ni hazina adimu ya elimu, ujuzi na maadili ya kitaaluma, ambayo jukumu lake ni kulinda uhai na afya ya binadamu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza Arafi, Mkuu wa Hawza nchini Iran, katika ujumbe wake wa kupongeza juhudi za madaktari amesisitiza kwamba; jumuiya ya wasomi wa udaktari na wahudumu wa afya ni hazina adimu ya elimu, ujuzi na maadili ya kitaaluma, ambayo hutekeleza jukumu lake la kulinda neema yenye thamani kubwa zaidi ya Mwenyezi Mungu, yaani uhai na afya ya mwanadamu.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

«وَمَنْ أَحْیَاهَا فَکَأَنَّمَا أَحْیَا النَّاسَ جَمِیعًا»

“Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote.”

(Surat Al-Maida, aya ya 32)

Jumuiya ya wasomi wa udaktari na wahudumu wa afya ni hazina adimu ya elimu, ujuzi na maadili ya kitaaluma, ambayo hutekeleza jukumu lake la kulinda neema yenye thamani kubwa zaidi ya Mwenyezi Mungu, yaani uhai na afya ya mwanadamu.

Udaktari katika mtazamo wa Tauhidi si mkusanyiko tu wa elimu na mbinu za kugundua na kutibu magonjwa; bali ni taaluma ya kibinadamu na jukumu la kimaadili, ambapo utafiti na uzoefu huunganishwa na kuheshimu utu wa mwanadamu, kuwaonea huruma wanaoteseka na kuwa waaminifu mbele ya uhai wa mwanadamu. Daktari, sambamba na kutumia mafanikio mapya ya kisayansi na teknolojia ya hali ya juu, anapaswa daima kuhifadhi heshima ya mwanadamu, matumaini ya mgonjwa na imani ya jamii.

Imam Ali (as) amesema:


«العِلمُ سُلطانٌ؛ مَن وَجَدَهُ صالَ بِهِ، ومَن لَم یَجِدْهُ صیلَ عَلَیهِ» 


Elimu ni mamlaka; mwenye kuipata hujipatia uwezo kupitia hiyo, na yule anayenyimwa elimu hiyo, wengine humtawala.”

Kwa hiyo, kuendeleza na kuinua taaluma ya udaktari nchini kunahitaji kuendelea kuzalisha elimu, kuendeleza tafiti za msingi na matumizi, kuimarisha elimu na mafunzo, kutumia kwa busara teknolojia mpya, na wakati huo huo kulinda maadili na haki katika huduma za afya.

Siku ya Madaktari ni fursa ya kuthamini juhudi za kielimu na kujitolea kwa dhati kwa madaktari ambao katika hospitali, vituo vya matibabu, vyuo vikuu na katika nyanja za utafiti na elimu, wanawahudumia wananchi kwa uwajibikaji na kujitolea.

Kwa kuwakumbuka kwa heshima mashahidi mashuhuri wa sekta ya afya na kutoa heshima kwa watumishi wote wa nyanja ya tiba, ninatoa pongezi zangu za dhati kwa jumuiya ya madaktari, maprofesa, watafiti, madaktari wanafunzi na wanafunzi wa udaktari, hususan madaktari wenye kujitolea na wanaofanya kazi kwa bidii katika Mji wa Qom na Chuo Kikuu cha Sayansi za Tiba cha Qom, kwa kuadhimisha siku hii.

Namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awape madaktari wote na wanaoshughulika katika nyanja ya afya mafanikio zaidi katika njia ya elimu na huduma, heshima na fahari, afya na ustawi; na kwa wagonjwa na wanaoteseka, naomba Mwenyezi Mungu awaponye haraka.

Alireza Arafi
Mkurugenzi wa Hawza Nchini Iran

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha