Alhamisi 13 Agosti 2026 - 15:09
Hafla ya Kumbukizi ya Kifo cha Mtume (saww) Yafanyika Dar es Salaam Tanzania + Picha

Hawza/ Waumini wa jijini Dar es Salaam jana tareh 28 Swafar 1448, walikusanyika katika Msikiti wa Ghadiir uliopo Kigogo Post jijini humo,  ili kushiriki katika maadhimisho ya Majlisi ya kumbukizi ya kufariki kwa Mtume Muhammad (saww).

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, majlisi hiyo iliongozwa na Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Maulana Hemed Jalala Mwakindenge, ambaye katika hotuba yake alielekeza fikra za waumini katika umuhimu wa mafundisho ya Mtume Muhammad (saww) na nafasi ya AhlulBayt wake (as) katika kuhifadhi, kufafanua na kuendeleza ujumbe wa Uislamu.

Mada kuu katika hafla hiyo ilikuwa ni: “Uislamu Umesimama Kupitia Mafundisho ya Mtume Muhammad (saww), na AhlulBayt Wake (as)”, ikiwa ni mada iliyowahitaji waumini kutafakari kwa kina juu ya msingi wa dini na mchango mkubwa wa Mtume (saww) pamoja na AhlulBayt wake (as) katika kuufikisha na kuuhifadhi ujumbe wa Mwenyezi Mungu.

Katika mawaidha yake, Maulana Hemed Jalala alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuyashikilia mafundisho ya Mtume Muhammad (saww) na kufuata njia ya AhlulBayt wake (as), hasa katika kipindi ambacho Umma wa Kiislamu unahitaji zaidi mshikamano, uelewa sahihi wa dini na kurejea katika misingi iliyowekwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Majlisi hiyo pia ilihudhuriwa na wageni na masheikh mbalimbali, jambo lililoipa hafla hiyo uzito na umuhimu wa pekee. Miongoni mwa wageni hao alikuwa Kiongozi wa Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Tanzania, ambaye alishiriki pamoja na waumini katika tukio hilo la kumuenzi Mtume Muhammad (saww).

Kumbukizi hiyo ilikuwa pia wakati wa kutafakari ukubwa wa pengo lililoachwa na kifo cha Mtume (saww). Kwa waumini, kukumbuka siku hiyo si kurejea tu katika historia ya zamani, bali ni kuhuisha huzuni ya kumpoteza kiongozi wa Umma na wakati huo huo kujikumbusha wajibu wa kuhifadhi ujumbe wake na kuufikisha kwa vizazi vijavyo.

Hafla ya Kumbukizi ya Kifo cha Mtume (saww) Yafanyika Dar es Salaam Tanzania + Picha

Hafla ya Kumbukizi ya Kifo cha Mtume (saww) Yafanyika Dar es Salaam Tanzania + Picha

Hafla ya Kumbukizi ya Kifo cha Mtume (saww) Yafanyika Dar es Salaam Tanzania + Picha

Hafla ya Kumbukizi ya Kifo cha Mtume (saww) Yafanyika Dar es Salaam Tanzania + Picha

Hafla ya Kumbukizi ya Kifo cha Mtume (saww) Yafanyika Dar es Salaam Tanzania + Picha

Hafla ya Kumbukizi ya Kifo cha Mtume (saww) Yafanyika Dar es Salaam Tanzania + Picha

Hafla ya Kumbukizi ya Kifo cha Mtume (saww) Yafanyika Dar es Salaam Tanzania + Picha

Maoni yako

You are replying to: .
captcha