Jumatatu 3 Agosti 2026 - 08:45
Israel yashambulia ghala la dawa karibu na Hospitali ya Mashahidi wa Al-Aqsa huko Ghaza

Hawza/ Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni alfajiri ya leo zililenga ghala la dawa lililokuwa karibu na Hospitali ya Mashahidi wa Al-Aqsa katika mji wa Deir al-Balah; shambulio ambalo limesababisha kuharibiwa kabisa ghala hilo na kuzuka kwa moto katika makumi ya mahema ya wakimbizi.

Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, kikinukuu Shirika la Habari la Anadolu, mashuhuda wa tukio walitangaza kuwa; ndege za kivita za utawala wa Kizayuni alfajiri ya leo zililishambulia kwa mabomu ghala la dawa katika eneo la Deir al-Balah, katikati mwa Ukanda wa Ghaza.

Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani, ghala hilo lilikuwa karibu na Hospitali ya Mashahidi wa Al-Aqsa na pembezoni mwa kambi ya mahema ya wakimbizi, na kufuatia shambulio hilo liliharibiwa kabisa. Aidha, makumi ya mahema yaliyokuwa makazi ya wakimbizi yaliteketea kwa moto au kuharibika.

Shambulio hilo limesababisha hofu kubwa miongoni mwa wagonjwa waliopo hospitali hiyo na wakazi wa kambi hiyo.l, wakazi wa eneo hilo waliiambia Anadolu kuwa jeshi la Israel lilitoa onyo la kuondoka eneo hilo dakika chache tu kabla ya kutekeleza shambulio.

Katika mwendelezo wa mashambulizi ya usiku ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Ghaza, Mpalestina mmoja amefariki kishahidi na watu wengine wanne wamejeruhiwa. Vilevile, jana, baada ya kutangazwa maelezo ya hatua ya pili ya makubaliano ya kusitisha mapigano, mashambulizi ya anga ya Israel yalisababisha Wapalestina wawili kuuawa kishahidi na kujeruhiwa watu wengine wasiopungua 21.

Kwa upande mwingine, Nikolay Mladenov, mwakilishi mkuu wa Baraza la Amani la Ghaza, alikuwa ametangaza hapo awali kuwa Harakati ya Hamas imekubali ramani ya kina ya njia ya kutatua hali ya Ghaza.

Aidha, Donald Trump, Rais wa Marekani, katika ujumbe aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii, alidai kuwa Baraza la Amani limefikia makubaliano kuhusu kunyang'anywa silaha Hamas na makundi mengine yenye silaha huko Ghaza.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha