Jumanne 15 Septemba 2026 - 17:24
Vikosi vya Wanajeshi wa Yemen vimewaachilia huru wafungwa waliokaa zaidi ya miaka 8 katika magereza ya Saudi Arabia

Hawzah/ Mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Masuala ya Wafungwa wa Yemen amesisitiza kwamba Vikosi vya Wanajeshi vya Yemen vimefanikiwa kuwaachilia huru baadhi ya wafungwa wa Yemen ambao walikuwa wametumia miaka mingi katika magereza ya adui wa Saudi Arabia na mamluki wake.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Ahmed Abu Hamraa, mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Masuala ya Wafungwa wa Yemen, katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Al-Masirah, amesisitiza kwamba; Vikosi vya Wanajeshi vimefanikiwa kuwaachilia huru baadhi ya wafungwa wa Yemen ambao walikuwa wametumia miaka mingi katika magereza ya adui wa Saudi Arabia na mamluki wake; miongoni mwao wapo wale ambao muda wao wa kuwa wafungwa ulizidi miaka minane, baada ya kuachiliwa kwao na kupokelewa rasmi na wananchi kwa mapokezi yanayostahili, wafungwa hao wamepata ari na morali ya juu.

Abu Hamraa ameeleza kwamba; wafungwa walioachiliwa walikuwa wametumia vipindi virefu vya kati ya miaka mitano hadi minane katika magereza, huku muda wa baadhi yao ukiwa umezidi miaka minane kutokana na kuendelea kushikiliwa na vikosi vya adui wa Saudi Arabia na mamluki wake, licha ya kuwepo kwa maelewano na makubaliano ya awali yaliyofikiwa kuhusu suala la wafungwa.

Amesema kwamba; kuwaachilia huru wafungwa hao kulitokea kupitia operesheni kubwa iliyotekelezwa na Vikosi vya Wanajeshi ya Yemen katika pwani ya magharibi; operesheni ambayo ilisababisha mabadiliko makubwa ya uwanja wa vita na kukombolewa  baadhi ya wilaya zilizokuwa chini ya udhibiti wa mamluki wa wavamizi, katika operesheni hiyo, Vikosi vya Wanajeshi viliweza kufikia magereza na jela ambazo wafungwa hao walikuwa wakishikiliwa na kuwaondoa humo.

Amebainisha kwamba; wafungwa hao hawakutarajia kwamba Vikosi vya Wanajeshi vingefanikiwa kuwafikia kwa namna hiyo, hususani baada ya miaka mingi waliyokuwa wamekaa nyuma ya nondo za magereza. Jambo hilo lilifanya wakati wa kuachiliwa kwao uwe mshangao mkubwa na furaha waliyokuwa wameisubiri kwa muda mrefu, baada ya kutumia miaka mingi wakiteseka katika mazingira magumu ya kizuizini.

Mjumbe huyo wa Kamati ya Kitaifa ya Masuala ya Wafungwa amesema kwamba; wafungwa hao walikabiliwa na mateso, kutendewa vibaya na ukiukaji wa haki mbalimbali wakati wa kipindi chao cha kizuizini. Hata hivyo, yale waliyofanyiwa na walinzi wao hayakuwazuia kudumisha ari na msimamo wao; kiasi kwamba baada ya miaka mingi ya kusubiri, walitoka magerezani wakiwa na morali ya juu na kurejeshewa uhuru wao.

Amekumbusha kwamba; suala la wafungwa lilikuwa na bado ni miongoni mwa masuala ya kibinadamu ambayo yanapaswa kushughulikiwa mbali na mahesabu ya kisiasa na kijeshi, hususani kwa kuwa makubaliano ya awali yaliyoafikiwa kwa upatanishi wa Umoja wa Mataifa yalielekeza kuchukuliwa hatua za kuwaachilia wafungwa, na mchakato wa kuwaachilia ulipangwa kufanyika mwezi Julai, lakini upande wa pili ulijiondoa katika ahadi zake na haukutekeleza yale yaliyokubaliwa.

Abu Hamraa amesema kwamba; kuwaachilia huru wafungwa hao kumefanyika kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na kutokana na juhudi za Vikosi vya Wanajeshi, baada ya kucheleweshwa na kukataa kutekeleza makubaliano kuwazuia kupata uhuru wao kupitia njia iliyokubaliwa. Vikosi vya Wanajeshi viliweza kuwafikia katika maeneo walikokuwa wakishikiliwa na kuwarejesha familia zao baada ya miaka mingi ya utumwa wa kifungo.

Ameongeza kwamba; wakati wa kuwapokea wafungwa hao walioachiliwa ulidhihirisha ukubwa wa furaha waliyoipata baada ya kutoka magerezani, walipokelewa rasmi na wananchi, huku kukiwa na uangalizi mkubwa kwa ajili ya kutambua na kuthamini miaka waliyotumia katika kifungo pamoja na mateso waliyoyapata katika kipindi cha kizuizini, mapokezi waliyopewa wafungwa hao yalikuwa katika kiwango kinachostahili kujitolea kwao na yale waliyovumilia katika miaka yao ya kifungo.

Taswira za kurejea kwao katika uhuru zilitawala juu ya athari za mateso waliyopitia, baada ya kujikuta wakiwa miongoni mwa wananchi wenzao, mbele ya familia zao na wenzao, badala ya kuwa ndani ya vizimba walivyotumia miaka mingi.

Abu Hamraa alisisitiza kwamba; wafungwa walioachiliwa walifika wakiwa na ari ya juu, licha ya mazingira magumu waliyopitia. Furaha ya uhuru pamoja na mapokezi ya wananchi na viongozi yalichangia kwa kiasi kikubwa kuondoa sehemu kubwa ya athari za miaka ya kizuizini. Kilichopatikana ni matokeo ya uvumilivu wa wafungwa kwa upande mmoja na juhudi zilizofanywa kwa ajili ya kuwaachilia kwa upande mwingine.

Amesema kwamba; mapokezi makubwa waliyopewa wafungwa hao yalithibitisha kuthaminiwa na wananchi wa Yemen kwa kujitolea kwao na uvumilivu wao, miaka ya kifungo haikupunguza ari yao; bali walirejea nchini kwao wakiwa na dhamira imara, baada ya kusubiri kwa muda mrefu siku ya kutoka magerezani na kurejeshewa uhuru wao.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha