Jumanne 15 Septemba 2026 - 16:23
Tunatahadharisha kwamba Serekali Imechukua Njia ya Kuipinga Dini

Hawzah/ Wanazuoni wa Bahrain wametoa taarifa ya pamoja, wakimuonya utawala wa Al Khalifa kuhusu njia ya ambayo umeichukua kupinga dini.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, wanazuoni wa Bahrain wametoa taarifa ambapo wameuonya utawala wa Al Khalifa kuhusu mwelekeo wa kuipinga dini ambao umeuchukua, na kusisitiza kwamba: “Tishio hili kubwa la kuwepo kwetu linaelekezwa wazi dhidi ya madhehebu, itikadi na alama za kidini.”

Maandishi ya taarifa hiyo ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

«إِنِ الْحُکْمُ إِلاَّ لِلَّـهِ أَمَرَ أَلاَّ تَعْبُدُوا إِلاَّ إِیَّاهُ ذلِکَ الدِّینُ الْقَیِّمُ وَلکِنَّ أَکْثَرَ النَّاسِ لا یَعْلَمُونَ»

“Hukumu si ya mwingine isipokuwa Mwenyezi Mungu, Ameamuru kwamba msimuabudu yeyote isipokuwa Yeye, hiyo ndiyo dini iliyonyooka, lakini watu wengi hawajui.”

Mambo ya mwanadamu na maisha yake hayawezi kusimama katika utaratibu, wala hali ya jamii yoyote haiwezi kuwa njema, iwapo njia yake imepotoka au inapingana na dini iliyonyooka ya Mwenyezi Mungu; sembuse ikiwa inapinga mojawapo ya itikadi, misingi, hukumu, sheria au alama zake za kidini.

Hii ni itikadi ya Kiislamu ambayo Waislamu wawili hawawezi kutofautiana juu yake, na Qur’ani Tukufu pamoja na Sunna Tukufu inayokubaliwa kwa pamoja vimeeleza wazi jambo hili.

Kwa msimamo wa kujali kwa dhati na kwa kina kuhusu nchi yetu pendwa ya Bahrain, ambayo katika historia yake yote haijawahi kuijua dini nyingine isipokuwa Uislamu, tunatoa onyo kali na kwa uwajibikaji kwamba utawala umechukua kwa kasi ya hatari njia inayopinga dini, huku ukiwa na tishio kubwa na la moja kwa moja dhidi ya uwepo wetu. Tishio hilo tunaliona wazi likielekezwa dhidi ya madhehebu, itikadi, alama za kidini na kila jambo linalotuhusu kwa upande wa dini. Hali hii inafanyika kupitia mfululizo wa miradi na maamuzi ya kimfumo ambayo kwa kasi inayoongezeka yamefikia kiwango cha tishio kubwa linaloiweka dini na itikadi katika hali ya hatari, jambo ambalo madhara yake yatakuwa mabaya kwa kila kitu nchini.

Miongoni mwa sura za mfululizo huu wa hatua ni kwamba utawala umeingilia Awqaf za Jaafaria, Husainiya, maeneo ya maombolezo, misikiti na makaburi yake; kiasi kwamba usimamizi wa maeneo hayo yote umewekwa chini ya baraza moja la serikali linaloongozwa na mmoja wa mawaziri wa serikali. Hatua hii inakiuka utaratibu ambao kwa miongo kadhaa ulikuwa umekubaliwa na kutekelezwa, kwamba masuala ya wakfu yawe huru kutokana na mamlaka ya siasa na sera zisizo za kidini.

Jambo limefikia hatua ambapo maamuzi ya baraza hilo yamekuwa ya lazima kutekelezwa mbele ya wasimamizi na wale walioteuliwa kusimamia wakfu, huku mamlaka ya kuwateua na kuwaondoa ikiwa imekabidhiwa kwa sera rasmi na hukumu zinazopingana na Sheria Tukufu. Hili linakiuka masharti yaliyowekwa na waqif pamoja na yaliyomo katika nyaraka zao za wakfu, ambazo kwetu zina hadhi ya matini ya kisheria inayolazimika kutekelezwa; kiasi kwamba hakuna mtu mwenye haki ya kuyavunja au kuyakwepa isipokuwa kwa kuwa na mamlaka ya wazi ya kisheria.

Hii ni hatua ya wazi na ya kiholela dhidi ya “wilaya ya kisheria”, ambayo uhalali wake unatokana pekee na mwenye kuweka wakfu na sharti lake, au kutoka kwa mtawala wa kisheria, wala si kutokana na uamuzi wa kiutawala au nguvu ya utekelezaji ya serikali. Hatua hii inakiwezesha chombo cha kisiasa kudhibiti hatma ya dini, alama zake za kidini na mali zake za wakfu, na inafungua mlango hatari wa kuzigeuza Nyumba za Mwenyezi Mungu na majlisi za maombolezo kuwa vituo vinavyotegemea serikali, vinavyofuata hesabu na maslahi yake na kuwa mbali na malengo ya wa'qif pamoja na hukumu za Sheria Tukufu.

Katika muktadha huo huo, uamuzi wao wa hivi karibuni wa kidhalimu umekuwa ni kuifunga na kuizuia hotuba ya kidini pamoja na sauti ya dini kwa ujumla katika nyanja zote za maisha, elimu, kujifunza, ulinganizi, mawaidha, mwito wa dini na kila kinachohusiana nayo; kiasi kwamba wameifanya yote hiyo kuwa chini ya masharti ya kupata kibali na leseni kutoka serikalini.

Hili lenyewe ni kuipinga dini na kuifanya dini kuwa chini ya udhibiti wa serikali, badala ya serikali kuwa chini ya dini, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyoamuru; Yeye ambaye hakuna kheri, maslahi wala uongofu isipokuwa kwa kumfuata na kuyaweka maisha kwa mujibu wa hukumu na sheria Zake.

Aidha, uamuzi huu unapingana na matakwa ya Katiba katika suala la uhuru wa kidini, pamoja na mila na desturi za nchi ambazo mizizi yake imejikita katika kina cha historia na ambazo zimerithishwa kutoka kizazi hadi kizazi, hususani katika uhuru wa misikiti, Husainiya na shughuli za kidini dhidi ya maamuzi, uingiliaji na matakwa ya sera zisizo za kidini. Bali uamuzi huu unaharibu na kunyang’anya uhalisia wote uliopo na uliorithishwa nchini unaohusiana na Uislamu na kuhifadhi uwepo na usafi wake.

Tunatoa wito wa kutumia busara na kufuta mfululizo wa maamuzi yanayoiwekea dini pingu na minyororo, kwa sababu mwisho wa hatua hizi bila shaka utakuwa wa kusikitisha na wenye kuleta maangamizi.

Hali ya nchi haiwezi kuwa njema isipokuwa kwa kushikamana na dini, kuhuisha hukumu zake na yale ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu ameyaamuru ndani yake kuhusu uadilifu na kuwapa watu haki zao za kisiasa na za maisha ambazo hawajanyimwa. Aidha, ni lazima kuhakikishwa kwa heshima na uhuru wa watu, ambavyo haviwezi kutenganishwa na heshima ya dini na uhuru wao wa kidini; wala si kwa kuwanyang’anya haki zao zaidi, kuikanyaga heshima yao na kunyang’anya mabaki ya nafasi ndogo ya dini waliyoachiwa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha