Jumanne 15 Septemba 2026 - 15:22
Bahrain yaendelea kuwafunga wanazuoni wa Kishia kwa lengo la kuufuta Ushia nchini humo

Hawzah/ Mahakama ya Bahrain imemhukumu Sheikh Abdulnabi Al-Nashaba, mwanazuoni wa dini wa Kishia, kifungo cha mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, mahakama moja ya Bahrain katika kikao chake cha Jumatano, tarehe 18 Shahrivar 1405 (9 Septemba 2026), ilimhukumu Sheikh Abdulnabi Al-Nashaba, mwanazuoni wa dini wa Kishia, kifungo cha mwaka mmoja kwa tuhuma zisizo na msingi. Mkuu wa Ofisi ya Mashtaka ya Al Khalifa alitangaza kwamba; Mahakama ya Jinai ya Mwanzo imetoa hukumu dhidi ya mshtakiwa, ikimhukumu kifungo cha mwaka mmoja cha taʿzir pamoja na kutaifisha simu yake ya mkononi.

Hali hii inajiri wakati ambapo taasisi nyingi za haki za binadamu pamoja na jumuiya za kisiasa zimelaani kuendelea kuwaita na kuwafikisha mahakamani baadhi ya wanazuoni, wahubiri na wasomaji wa nauha na maulidi na mamlaka za Bahrain, kutokana na shughuli zao za kidini. Taasisi hizo zimeeleza kuwa hatua hizi ni sehemu ya kampeni rasmi inayolenga kuzuia uhuru wa utoaji mafundisho na tafiti za kidini, kukandamiza uhuru wa kidini na kutumia njia za kibaguzi dhidi ya Mashia nchini Bahrain.

Inafaa kutajwa kwamba vikosi vinavyohusishwa na utawala wa Al Khalifa, Jumatano tarehe 19 Agosti 2026 (28 Mordad 1405), baada ya kuvamia nyumba ya Sheikh Abdulnabi Al-Nashaba katika mji wa Al-Zahra (sa), vilimkamata na kumpeleka mahali pasipojulikana. Hatua hiyo ilichukuliwa bila kibali chochote cha mahakama wala kutangazwa kwa sababu za kukamatwa kwake. Wakati huo huo, vyanzo vya ndani vinakadiria kwamba huenda sababu ya kukamatwa Sheikh Al-Nashaba ni uchochezi wa kimadhehebu uliofanywa na baadhi ya watu waliopewa uraia wa Bahrain, kwa lengo la kuondoa Ushia nchini Bahrain, dhidi ya Sheikh Al-Nashaba. Inadhaniwa kwamba watawala wa Bahrain, kwa kushirikiana na Israel, wameanza mchakato wa kuuondoa Ushia nchini Bahrain hatua kwa hatua.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha