Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, khitma hiyo inayoendelea muda huu katika Msikiti wa BAKWATA Makao Makuu, Kinondoni, Dar es Salaam, huku waombolezaji, viongozi wa dini na wageni mbalimbali wakikusanyika kwa ajili ya kumuombea marehemu na kuungana na familia katika kipindi hiki cha majonzi na huzuni.
Uwepo wa Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania, Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge, umeendelea kuakisi umoja na mshikamano wa viongozi wa dini katika kushirikiana kwenye nyakati muhimu za kijamii, hususan wakati wa majonzi, ambapo dua na maombi huleta faraja kwa wafiwa na kuwaunganisha Waislamu katika ibada na huruma.
Miongoni mwa viongozi wa dini waliohudhuria kwenye khitma hiyo ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani, Dkt. Alhad Salum Mussa; Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Abbas Ramadhani; pamoja na Imam wa Msikiti wa Majema na mjumbe wa Baraza la Ulamaa la BAKWATA, Sheikh Hamid Masoud Jongo, sambamba na masheikh na wageni wengine mbalimbali.
Khitma hiyo imekuwa pia ni sehemu ya kuendeleza dua na kumuombea marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan, huku viongozi na waumini wakimwomba Mwenyezi Mungu amsamehe makosa yake, amrehemu na amuweke mahala pema katika Akhera, pamoja na kuipa familia yake subira, nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu cha kumpoteza mpendwa wao.







Maoni yako