Jumapili 20 Septemba 2026 - 01:59

Hawza/ Kwa mtazamo wa Qur’ani na Ahlul-Bayt (as), kile ambacho watu duniani wanakifanyia juhudi ili kukipata si chochote isipokuwa “hutam”; yaani, mali ya muda mfupi na inayotoweka, ambayo ni kama mabaki ya vitu vilivyokauka vinayotawanywa na upepo na kutoweka, Nukuhu ya Imam Shahidi kutoka katika maneno ya Imam Sajjad (as) inasisitiza kuhusu dunia kutokuwa na thamani na kumtahadharisha mwanadamu dhidi ya kudanganywa na matwa'ghuti.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, katika ufafanuzi wa Hadithi ya Imam Shahidi, kwa kurejea maneno ya Imam Sajjad (as) kuhusu matwa'ghuti na wafuasi wao, kuna tahadhari dhidi ya kudanganywa na mwonekano wa mambo ya kidunia; kwa sababu kushikamana na dunia, fedha, utajiri, heshima ya nje na hadhi ya kijamii, vimetajwa kuwa miongoni mwa sifa za watu duniani, Matini ya maelezo haya inawasilishwa kwenu, enyi wasomi na watu wenye uelewa.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

Ni maandishi ya Imam Sajjad, salamu za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kwa mujibu wa yaliyopokelewa kutoka kwa Abu Hamzah Thumali:

«أیها المؤمنون لا یفتننکم الطواغیت وأتباعهم.»

“Enyi waumini! Matw'aghuti na wafuasi wao wasikudanganyeni.”

Wafuasi wao, katika daraja la kwanza, ni watu wao wa karibu na wale wanaowazunguka; na baada ya hapo ni lile kundi kubwa la watu linalojifunga kwa tw'aghuti, linamfuata na kwenda nyuma yake; bila kufanya uchunguzi, bila kuhisi wajibu na bila kujihusisha kwa kujitolea. Wanaokusudiwa kuwa wafuasi wao ni watu wa aina hii.

Kisha Imam Sajjad (as) anataja sifa mbalimbali za matwa'ghuti na wafuasi wao.

«مِن أهلِ الرَّغبةِ فی هذه الدنیا»

“Sifa ya kwanza ya watu hawa, na huenda ndiyo sifa yao muhimu zaidi, ni kwamba wao ni watu wa dunia na wanaipenda dunia.”

«المائلون إلیها»

“Wanaielekea dunia.”

«المفتتنون بها»

“Wanaipa umuhimu na kuvutiwa nayo”; maana yake ni kwamba mtu ambaye yuko kinyume na watu hawa, hata hapaswi kuipa dunia umuhimu.

«المقبلون علیها و علی حطامها الهامد»

“Hutam” maana yake ni vipande vya mabaki ya vitu vilivyokauka, kama vipande vya miti na vitu vya aina hiyo, kila kitu mnachokiona katika dunia hii; fedha zake, utajiri wake, heshima yake ya nje, hadhi yake ya kijamii; vyote hivi ni kama vile vipande vya miti vilivyotawanyika ardhini.

«حطامها الهامد»

“Hāmidi” maana yake ni kitu kilichokwisha na kuzimika, moto unapozimika, husemwa “hamada”, yaani umeangamia, mwali wake umepungua na kumalizika, hivyo, hutam hii ni kitu ambacho kiko katika hali ya kutoweka, na sifa ya kutoweka ni sehemu ya asili yake.

«و هشیمها البائد»

“Hashīm” pia ina maana ya vitu vilivyokauka, vilivyovunjika-vunjika na kutawanyika, kama ilivyokuja katika Qur’ani Tukufu:

«هَشِیماً تَذْرُوهُ الرِّیاحُ»

“...yakawa mabaki makavu yanayotawanywa na upepo.”

(Suratul-Kahf, Aya ya 45)

Hivi ndivyo ilivyo kwa mabaki madogo-madogo yanayoanguka ardhini; upepo unapokuja, hata kama ni upepo mwanana, hukusanya vitu hivyo na kuvipeleka pamoja nao.

Vitu vyote hivi ambavyo watu duniani wanavyo na kujitesa sana kwa ajili yake, kwa mtazamo wa hekima wa Qur’ani na Ahlul-Bayt (as), vyote hivyo ni “hashīm”.

«و هَشیمُها البَائد غداً»

“Na hashīm yake ambayo kesho itakuwa imetoweka.”

Upepo umefika na kuichukua; yaani imeangamia.

Sifa ya matwa'ghuti ni kwamba wanafanya kazi kwa ajili ya dunia; kwa ajili ya mambo haya ambayo kwa mtazamo wao yanaonekana kuwa makubwa, lakini kwa hakika hayana thamani, wanatumia juhudi zao zote.

Hawa wasikudanganyeni.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha