Jumamosi 19 Septemba 2026 - 08:13
Faida za Kuleta Ukaribu na Upendo Miongoni mwa Waumini

Hawza/ Imam Muhammad Baqir (as), katika riwaya moja, ameeleza umuhimu wa kujenga uhusiano wa upendo, ukaribu na huruma miongoni mwa waumini.

Shirika la Habari la Hawza, limechapisha riwaya ifuatayo kutoka katika kitabu cha «Al-Kafi».

Imam Muhammad Baqir (as):

«رَحِمَ اللهُ امرَءاً ألَّفَ بَینَ وَلِیَّینِ لَنا، یا مَعشَرَ المُؤمِنِینَ، تَألَّفُوا وتَعاطَفوا.»

“Mwenyezi Mungu amrehemu mtu ambae amepatanisha na kuleta uhusiano wa upendo baina ya watu wawili miongoni mwa marafiki zetu. Enyi waumini! Jengeni ukaribu na maelewano baina yenu, na muhurumiane.”

Al-Kafi, Juzuu ya 2, uk. 345.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha