Mwenye kula mali ya nduguye kwa dhulma na asimrudishie mwenyewe, basi chakula chake Siku ya Kiyama ni miali ya moto.
Mlipe kibarua kabla jasho lake halijakauka.
Mche (muogope) Mwenyezi Mungu na sema haki hata kama utaangamia, kwani (kwa hakika) kuokoka kwako kuko katika hilo. Mche Mwenyezi Mungu na acha batili hata kama kuokoka kwako kuko katika hilo,…