Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ibrahim Zakzaky alitoa hotuba jioni ya Jumanne, tarehe 27 Safar 1448, inayolingana na tarehe 20 Mordad 1405, katika hafla ya kufunga mkutano wa siku mbili, wa awamu ya 18, uliofanyika mjini Abuja.
Kiongozi huyo wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria alisema katika hafla hiyo: Ujumbe wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) katika kila zama ni ujumbe wa uongofu na njia ya wokovu.
Aliongeza: Yanayotokea leo duniani, katika baadhi ya vipengele yanafanana na hali iliyokuwepo katika zama za Mtume Mtukufu (saww), na sifa na tabia za waumini, wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu na wanafiki zimejitokeza wazi miongoni mwa watu.
Sheikh Zakzaky, akizungumzia hali ya sasa ya dunia, alisema: Leo dunia imegawanyika katika pande mbili; upande wa wale wanaomfuata Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (saww), na upande wa Magharibi ambao ni wawakilishi wa Shetani.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, akizungumzia kuandaliwa kwa maadhimisho ya kuzaliwa kwa Mtume Mtukufu (saww) mwaka huu, alisisitiza umuhimu wa kutumia fursa hizo kuwawezesha Waislamu kukaribiana zaidi na kuongeza uelewa wa umma kuhusu mabadiliko na masuala yanayoendelea duniani.
Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria alifafanua kwa kusema: Kukaribiana na kuwasiliana huku baina ya watu kunaondoa kuta za utengano na mifarakano.
Sheikh Zakzaky pia, akikumbusha kumbukumbu ya kufariki dunia kwa Mtume Mtukufu (saww) tarehe 28 Safar, alitoa salamu za rambirambi kutokana na msiba huo na kubainisha kwamba; kumkumbuka Mtume wa Rehema (saww) na kuandaa maombolezo kwa ajili yake ni miongoni mwa njia za kuhuisha dini.
Mwisho, alisisitiza kwamba; lengo la kukumbuka matukio haya si kuomboleza pekee, bali ni kujifunza na kupata mazingatio kutokana na matukio ya maisha ya Mtume Mtukufu (saww) na mwenendo wake, kisha kuyatekeleza katika maisha ya leo.
Maoni yako