Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza Arafi, katika khutba za Swala ya Ijumaa ya tarehe 16 Mordad 1405, (August 7 2026) zilizofanyika katika Muswalla wa Quds mjini Qom, amesema: “Vita vya hivi karibuni na uwanja huu mkubwa wa muqawama wa kistaarabu vilibeba masomo ya kimataifa.”
Somo la kwanza: Kuporomoka kwa maadili katika ulimwengu wa sasa
Imam wa Swala ya Ijumaa ya Qom amesema: “Kuporomoka kwa mfumo wa maadili katika ulimwengu wa sasa na maadui wa mataifa kuvuka mipaka ya thamani na vigezo vyote vya kimaadili ni somo la kwanza.” Uchunguzi wa historia unaonesha kwamba; hadi sasa ubinadamu haujawahi kufikia kiwango hiki cha kuyumba kimaadili, nguvu zinazotawala rasilimali na uwezo wa mwanadamu zimeachwa bila hata sifa za msingi za kimaadili.
Ameendelea kusema: “Mwananadamu anapaswa kulia; watu wameonesha kuchukizwa na kujitenga na hali hii, watu barani Ulaya na Marekani wameonesha kuchukizwa na hali hiyo, lakini hii ni sauti ya wananchi ambayo haikufika popote, nguvu za kishetani zimeendelea na mlolongo wao wa dhuluma, na mfumo wa maadili wa dunia umeanguka, dunia iko katika ukingo wa mabadiliko mengine.”
Somo la pili: Kuporomoka kwa mfumo wa kisheria na kimataifa
Khatiibu wa Swala ya Ijumaa ya Qom amesema: “Taasisi kama Baraza la Usalama na nyinginezo zimekaa kimya mbele ya dhuluma au zimekuwa pamoja na madhalimu, Baada ya Vita vya Pili vya Dunia, mifumo hii iliandaliwa ili angalau kiwango fulani cha haki kitawale duniani, lakini hilo halikuwahi kutimia, hata hivyo, kwa namna inayoonekana wazi, mifumo yote ya kisheria na kimataifa imeporomoka, na madikteta wa dunia wameugeuza ulimwengu kuwa msitu ambao nguvu ndiyo inayotawala.”
Somo la tatu: Kufichuka kwa sura halisi ya Marekani na Wazayuni
Amesema: “Hapo zamani, sura halisi ya uhalifu ya Marekani na Wazayuni haikuwa imefichuka, na ilikuwa lazima ifafanuliwe kwa kila mtu, lakini leo, sura halisi ya mbwa hawa inawashambuliwa kote, hata marafiki zao wenyewe, kuwadhuru watoto, kuwaua watoto, mauaji ya kimbari, kushambulia miundombinu na ukatili uliokithiri dhidi ya makundi yote, ya kijeshi na yasiyo ya kijeshi, katika eneo lote, ni miongoni mwa ukweli ulio wazi wa Marekani.”
Somo la nne: Kukosekana kwa uaminifu katika aina yoyote ya mazungumzo
Mkuu wa Vituo vya Hawza nchini Iran ameongeza: “Hapo zamani, maadui wakubwa walikaa pamoja na kuzungumza, na kulikuwa na kiwango cha chini cha vigezo katika mazungumzo, lakini ulimwengu mzima umeona kwamba wahalifu hawa walikiuka ahadi na mikataba yao ya kwanza, matokeo yake ni kwamba haiwezekani kuwaamini katika kauli zao, Ikiwa mtu ataamini maneno yao, basi ima ni kwa sababu ya kutokuwa na uelewa au ni kwa sababu ya nia mbaya.”
Somo la tano: Usalama wa kukopeshwa hauna faida
Khatiibu wa Swala ya Ijumaa ya Qom amesema: “Serikali za eneo hili zimeelewa kwamba usalama wa kukopeshwa na kuombaomba usalama kutoka kwa Marekani hauna faida.”
Akiyaelekea mataifa ya eneo hilo amesema: “Maadamu mtakuwa pamoja na maadui wa Uislamu na Iran, ngurumo za makombora yetu zitakuwa tishio kwenu.”
Somo la sita: Kasri la vioo la Marekani
Imam wa Swala ya Ijumaa ya Qom ameongeza: “Ubinadamu unapaswa kujua kwamba Marekani iko katika kasri la vioo, Marekani imejenga majumba mazuri juu ya mchanga unaohama, ambayo misingi yake ni dhaifu, licha ya sauti zote ambazo Marekani inazo, dunia imeona kwamba Marekani imeshindwa mbele ya Iran, mhimili wa muqawama na Taifa la Iran.”
Somo la saba: Taifa la Iran halitarudi nyuma kamwe
Ameongeza: “Netanyahu, Trump na washirika wao wanapaswa kujua kwamba taifa hili linalotaka kulipiza kisasi na linalokesha usiku kwa ajili ya malengo ya Uislamu, bado limesimama kidete kwa ajili ya Uislamu, Mapinduzi, Uongozi na majeshi ya Iran, na kamwe halitarudi nyuma.”
Somo la nane: Dunia imetambua thamani ya muqawama
Ayatullah Arafi amesisitiza: “Dunia imetambua thamani ya muqawa.a wenye hekima, maadui walitamani sisi tusalimu amri, lakini wameyapeleka matamanio hayo kaburini, adui anapaswa kusalimu amri mbele ya haki, kisasi cha damu ya Kiongozi shahidi wa Mapinduzi na mashahidi wa Iran na wa muqawama kinawasubiri.”
Amekumbusha kuwa: “Taifa hili litaendelea na njia hii, Kuendelea na njia hii katika mazingira nyeti ya leo kunahitaji uelewa, busara, ujasiri na uwepo katika uwanja wa tukio, Maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia, kuwa pamoja kimalego na kijamii kwa ajili ya malengo makubwa, pamoja na muungano mtakatifu huku Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei akiwa neno la mwisho la uamuzi, ni miongoni mwa masharti hayo.”
Nguvu za kijeshi ni hitaji la uhai wa leo
Mkuu wa Vituo vya Hawza nchini Iran, ameendelea kusema: “Nguvu za kijeshi, kiusalama na za silaha ni jukumu la majeshi, vyuo vikuu na serikali, nguvu za kijeshi ni hitaji la uhai wa leo, wale waliokuwa wakipuuza nguvu za kijeshi walikuwa wakikosea, usimamizi wa kijihadi ni sharti jingine la kuendelea na njia hii, taifa nalo linapaswa kushirikiana.”
Nguzo mbili muhimu katika muqawama
Ayatullah Arafi, katika khutba ya kwanza, akieleza kwamba; muqawama na jihadi vinahitaji nguzo mbili muhimu, amesema: “Nguzo ya kwanza ni heshima na kujivunia mtu binafsi na jamii wakati wa kukabiliana na adui, hisia ya kujiheshimu katika nyanja pana za kijamii ni sharti muhimu la muqawama na kujilinda dhidi ya wageni.”
Alieliielezea subira na uvumilivu mbele ya matatizo yanayopatikana katika njia ya kuilinda nchi na malengo ya Mwenyezi Mungu, na kuongeza: “Muqawama unategemea nguzo hizi mbili za kisaikolojia na za ndani, muqawama na kuwepo katika uwanja wa ulinzi na jihadi, kwa upande mmoja, unahitaji heshima ya pamoja ndani ya jamii, na kwa upande mwingine unahitaji subira na ustahimilivu katika kukabiliana na matatizo.”
Subira ni kanuni ya kimantiki
Khatiibu wa Swala ya Ijumaa ya Qom, huku akieleza kwamba; subira mbele ya vikwazo na matatizo ni kanuni ya kimantiki, amesema kwa msisitizo: “Taifa ambalo lina sifa hizi haliwezi kushindwa, na litashinda mbele ya adui.”
Subira ni sababu ya kuchanua na kustawi
Amesema: “Uvumilivu na subira ni sharti kuu la kufikia malengo na matarajio makubwa, Jambo hili limetajwa katika Aya na riwaya nyingi; kwa mfano, neno ‘subira’ limetumika ndani ya Qur’ani zaidi ya mara mia.”
Subira ni tegemeo la mifumo ya Sheria
Mkuu wa Hawza ameendelea kusema: “Subira ni tegemeo la mifumo yote ya Sheria, Katika riwaya imetajwa subira mbele ya misiba, subira katika kutekeleza utiifu na subira katika kuacha maasi.”
Aina mbili za subira
Akiashiria kwamba subira imegawanyika katika makundi mawili, ameongeza: “Aina ya kwanza ya subira ni mbele ya matukio ambayo hayako chini ya hiari ya mwanadamu na ambayo binadamu huyapitia; lakini aina ya pili ni subira ya hiari, ambayo inahusu kutekeleza majukumu ya Mwenyezi Mungu na kuacha maasi.”
Imam wa Swala ya Ijumaa ya Qom ameongeza: “Subira ya pili ni uvumilivu ambao tunauchagua kwa ajili ya kupata saada na maendeleo, ili tukabiliane na matatizo kwa kuyakabili moja kwa moja.”
Amesema: “Wakati mwingine jambo hutokea na tunapaswa kuwa na subira, lakini wakati mwingine tunaamua kwamba, kwa ajili ya kutekeleza majukumu yetu ya Mwenyezi Mungu na ya kijamii, tuingie katikati ya matatizo na kuwa na subira, hii ndio subira hai na uvumilivu uliochaguliwa.”
Khatiibu wa Swala ya Ijumaa ya Qom amesema: “Subira ya mtu binafsi ni ile subira ambayo tunavumilia ugumu kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya kibinafsi kama vile Swala na kadhalika. Lakini subira ya kijamii ni jambo ambalo subira ya hiari inakuwa sehemu ya utamaduni wa jamii, na watu wote wa jamii wanakabiliana na hatari bila kuogopa wala kupoteza moyo mbele ya hatari hizo.”
Akiashiria kwamba katika fasihi ya leo, subira hai na ya kijamii hutajwa kwa jina la muqawama, amekumbusha: “Muqawama una maana ya subira kubwa, yenye upeo mpana, hai, ya kijamii na iliyopangwa, pamoja na kuzikabili hatari kubwa kwa ajili ya malengo makubwa ya uhuru wa taifa na Umma.”
Dhana ya muqawama
Ayatullah Arafi amesema: “Maimamu wawili wa Mapinduzi wameongeza maneno na dhana nyingi katika fasihi ya Iran na dunia, na miongoni mwa hizo ni dhana ya muqawama ambayo katika ulimwengu wa Kiislamu imegeuka kuwa nadharia. Muqawama ni subira yenye hekima, ya kijamii na hai kwa ajili ya kutimiza malengo makubwa; na taifa letu limeuchagua kwa ajili ya kutimiza malengo makubwa na kuelekea katika ustaarabu mpya wa Kiislamu.”
Maoni yako