Jumapili 9 Agosti 2026 - 22:15
Ombi la Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Mashia wa Lebanon kwa Serikali ya Nchi Hiyo

Hawzah/ Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Mashia wa Lebanon ameiomba serekali ya Lebanon, kutokana na mkwamo uliopo katika mazungumzo na kushindwa kwa chaguo zake, kufungua milango ya mazungumzo na makundi mbalimbali ya Walebanon, hususan Muqawama.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ali Al-Khatib, Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Mashia wa Lebanon, ameiomba serikali ya Lebanon, kutokana na mkwamo uliotokea katika mazungumzo na kushindwa kwa madai yake, kufungua milango ya mazungumzo na makundi na vyama mbalimbali vya Lebanon, hususan Muqawama, kwa lengo la kufikia mwafaka wa kukabiliana na hatua inayokuja.

Aliwataka Walebanon wote katika hatua hii kutumia hekima na busara ili kuzuia fitina ambayo kwa sasa inahofiwa zaidi kuliko adui wa Israel. Alitahadharisha dhidi ya kulengwa kwa Syria na kusema: Syria ambayo tuna wasiwasi juu yake, si kwamba tunaihofia; na kwa kiwango kilekile tunachojali kuhusu Lebanon, tunaijali pia Syria, na tunaunga mkono wito wa kufungua ukurasa mpya na Damascus.

Arubaini ni fursa ya kufufua mapambano ya Imam Hussein (as) kwa ajili ya kuurekebisha Umma na kukabiliana na ufisadi uliojaa kwa Umma

Sheikh Al-Khatib alirejelea Arubaini ya kuuawa kishahidi Imam Hussein (as) huko Karbala na mkusanyiko wa mamilioni ya watu ambao Iraq hushuhudia kila mwaka katika tukio hili, na kusema: Hili si tukio la kidini la Kishi'a pekee, bali ni kufufua mapambano ya Imam Hussein (as) kwa ajili ya kuurekebisha Umma na kukabiliana na ufisadi ambao umeula na kuuharibu mwili wa Umma.

Alisema: Mapambano ya Imam Hussein (as) hayakuwa kwa ajili ya kugombania utawala na Bani Umayya, bali yalikuwa kwa ajili ya kufanya marekebisho. Kwa sababu hiyo, Maimamu (as) walifufua mapambano ya Ashura ili malengo yake yadumu katika dhamiri ya Umma, hivyo kufufuliwa kwa tukio hili huko Karbala kunafanyika ndani ya mfumo huo.

Aliendelea kusema: Kinachoendelea leo ni Magharibi kuuzuia Umma kutekeleza nafasi yake, kwa ajili ya kufikia malengo yake maovu.

Kushindwa kwa mazungumzo na utawala wa Kizayuni

Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Mashia wa Lebanon alizungumza kuhusu hali ya kisiasa ya Lebanon na eneo hilo, na kusema: Jana, duru ya mazungumzo kati ya uongozi wa Lebanon na utawala wa Kizayuni ilimalizika, kama ilivyotarajiwa, bila kupata matokeo yoyote; kwa sababu adui wa Israel aliendelea kushikilia misimamo yake ya kukataa kujiondoa katika ardhi ya Lebanon, na akashikilia kisingizio cha kufanya uhakiki wa eneo la majaribio katika eneo ambalo hapo awali alidai kuwa amejiondoa.

Wakati uongozi wa Lebanon ulikuwa ukiitegemea Serikali ya Marekani kuweka shinikizo kwa utawala wa Kizayuni, Serikali hii ya Marekani haikujisumbua kufanya hivyo; hivyo, kwa masikitiko, Lebanon ilitoka katika duru hii mikono mitupu, kwa sababu Marekani yenyewe inaunganisha njia ya Lebanon na mgogoro wa eneo hilo, na inaitumia Lebanon kama karatasi ya shinikizo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Tahadhari kuhusu matukio yajayo

Aliongeza kusema: Enyi ndugu, si jambo lililofichika kwa yeyote kwamba hali ya Lebanon imefungamana kwa kiasi gani na yale yanayotokea katika eneo hili, kiasi kwamba uhusiano kati ya njia hizi mbili umekuwa jambo lililo wazi; hususan katika kipindi cha uchaguzi wa Marekani na Israel, ambapo maslahi binafsi hutangulizwa kuliko maslahi ya umma.

Kwa hiyo, tunapaswa kusubiri miezi ijayo ili mambo yaanze kujidhihirisha. Hata hivyo, hatua inayokuja ni nyeti na ya muhimu, na huenda adui akachukua hatua zisizopimwa; kwa hiyo, tunapaswa kuwa tayari kwa uwezekano wote.

Kushindwa kwa Marekani katika kukabiliana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kunaweza kuisukuma Serikali ya Marekani kuchukua hatua za kichaa, wakati Serikali ya utawala wa Israel inafanya kila juhudi kuongeza hali ya mvutano ili kukwepa yale ambayo tafiti za maoni zinatabiri kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Israel.

Sheikh Al-Khatib aliendelea: Kwa sababu hiyo, wito wetu wa kudumu kwa Walebanon wote ni kutumia hekima na busara katika hatua hii na kuepuka mivutano na uchochezi, ili kuzuia fitina ya ndani ambayo tunaikhofia zaidi kuliko hofu yetu dhidi ya adui.

Aliendelea kusema: Hapa, jukumu la kwanza na kubwa liko juu ya uongozi wa Lebanon, tumekuwa tukiuomba na tunaendelea kuuomba kwamba baada ya kushindwa kwa chaguo lake, upitie upya msimamo wake na kufungua milango ya mazungumzo miongoni mwa Walebanon, hususan na Muqawama wenyewe.

Jukumu hili hasa ni la Rais, ili kufikia mwafaka wa kukabiliana na hatua inayokuja, kwa sababu umoja miongoni mwa Walebanon ndio kizuizi pekee kisichopenyeka cha kukabiliana na mizigo ya hatua ijayo.

Wito wa kuunda mwavuli wa kiusalama wa kikanda

Sheikh Al-Khatib aliongeza: Katika ngazi ya kikanda, hakuna mtu anayepaswa kudhani kwamba katika kivuli cha jeuri ya Marekani na Israel, yuko nje ya kulengwa. Kwa hiyo, tumeziomba nchi za Kiarabu na Kiislamu zenye ushawishi katika eneo hili, hususan Saudi Arabia, Misri, Uturuki na Syria, kuunda mwavuli wa kisiasa na kiusalama wenye uwezo wa kuzuia na kukabiliana na malengo ya Israel, na kuratibu suala hili pamoja na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Alisisitiza: Katika suala hili, tunaonya dhidi ya juhudi za kuwanyanyasa au kuwadhulumu walio dhaifu ndabi ya nchi hizi, kama ambavyo Iran imekuwa ikilengwa peke yake, kwa dhana ya baadhi ya watu kwamba kufanya hivyo kunatimiza maslahi yao. Katika suala hili, hatufichi hofu yetu kuhusu Syria, tukizingatia hali halisi ambayo inaishi ndani yake, jambo kuu likiwa ni uvamizi wa Israel kusini mwa Syria. Tunalaani kwa maneno makali zaidi milipuko inayotokea nchini Syria.

Sheikh Al-Khatib alisema: Kwa kiwango kilekile tunachojali kuhusu Lebanon, tunajali pia kuhusu Syria na tuna wasiwasi juu yake, si kwamba tunaiogopa, kama baadhi wanavyojaribu kuonesha. Kwa hiyo, tunaunga mkono na kuukaribisha wito wa Spika wa Bunge la Lebanon, Nabih Berri, na Katibu Mkuu wa Hezbollah, Sheikh Naim Qassem, wa kufungua ukurasa mpya na Serikali ya Syria wakati mwafaka utakapofika.

Msimamo wa Kimsingi Kuhusu Umoja

Alibainisha: Msimamo wetu bado unatokana na kujali kwetu na kushikamana kwetu na msingi wa “Umma”, kwa sababu sisi hatujioni kuwa ni wachache na tunakataa kuitwa hivyo, hapo awali tulikataa fikra za kujitenga kisiasa na kijamii, na tunaendelea kuzikataa sasa na tutazikataa pia katika siku zijazo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha