Jumapili 9 Agosti 2026 - 20:15
“Makubaliano ya Kimfumo” Hayana Manufaa kwa Lebanon

Hawzah/ Hussein Jashi amesema: “Makubaliano ya Kimfumo” hayana manufaa kwa Lebanon, kwa sababu hayajabadilisha mwelekeo wa mapambano dhidi ya adui Mzayuni.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza,, Hezbullah katika mji wa Dardghaya, kusini mwa Lebanon, iliandaa hafla ya maombolezo kwa ajili ya “roho za mashahidi wa Muqawama wa Kiislamu.” Katika hafla hiyo, Hussein Jashi, mwakilishi wa Kambi ya “Uaminifu kwa Muqawama” katika Bunge la Lebanon, alihudhuria pamoja na familia za mashahidi, wanazuoni wa dini, watu mashuhuri wa kijamii na wananchi kwa wingi.

Baada ya kusoma aya za Qur’ani Tukufu, Hussein Jashi katika hotuba yake alirejelea “Makubaliano ya Mfumo” (Ittifaq al-Iṭār) yaliyoafikiwa kati ya Lebanon na Israel. Akiuliza iwapo makubaliano hayo yana manufaa kwa Lebanon au la, aliongeza: “Katika suala hili, sisi tuna mtazamo tofauti nanyi, Joseph Aoun, Rais wa Lebanon, na Nawaf Salam, Waziri Mkuu wa Lebanon, wanasema makubaliano haya yana manufaa kwa Lebanon, lakini sisi tunasema hapana, hayana manufaa kwa Lebanon.”

Kupambana na Wazayuni ni vita halisi na ya kiitikadi

Alisema: “Makubaliano ya Mfumo” hayana manufaa kwa Lebanon, kwa sababu hayajabadilisha mwelekeo wa muqawama dhidi ya adui Mzayuni; kwa sababu kwa mtazamo wetu wao ni adui wa uwepo wetu, na kupambana nao ni vita ya asili na ya kiitikadi. Wao ni wavamizi na wanyang’anyi wa ardhi za Wapalestina, Wayahudi, Wakristo na Waislamu. Tatizo letu si pamoja na Wayahudi wa asili wa Palestina, bali tatizo letu ni pamoja na wale waliotoka nje na kuishi katika ardhi hii, wao ni wanyang’anyi wa ardhi hii, zaidi ya hayo, adui Mzayuni ana tamaa za siri na dhahiri dhidi ya Lebanon.

Mjumbe huyo wa Kambi ya Muqawama aliongeza: Ikiwa tutasoma historia ya Wazayuni, tutaona kwamba katika kipindi cha miaka arobaini au hamsini iliyopita hawajawahi kuficha tamaa zao. Kwa mfano, Benjamin Netanyahu mara kadhaa amewasilisha ramani inayoitwa “Israel Kubwa”, ambayo inajumuisha eneo lote la Lebanon, na amesema kwamba ana jukumu la kiroho la kuunda Israel Kubwa, Kwa hiyo Lebanon inakabiliwa na hatari ya kuwepo kwake, na hatuwezi kulishughulikia suala hili kana kwamba halipo.

Baadaye makubaliano yalifikiwa kati ya Lebanon na adui Mzayuni, kwa namna ambayo mapambano dhidi ya adui huyo yangehitimishwa kwa malipo ya amani; na hilo likiwa kwa sharti la kunyang'anywa silaha za Muqawama zinazomtishia Israel. Uadui wetu dhidi yao una mizizi na uko wazi; walifanya uvamizi mwaka 1948, wakafanya mauaji ya halaiki huko Hula, na baadaye katika miaka ya 1978 na 1982 pia walifanya uhalifu; miongoni mwao ni tukio la Msikiti wa Al-Abbasi, ambapo watu 120 waliuawa kishahidi.

Jashi aliendelea kusema: Ikiwa adui huyu kimsingi ni adui mvamizi ambaye aliishambulia Lebanon katika miaka ya 1968, 1969 na 1973, na ikiwa wakati huo hakukuwa na Muqawama, Hezbollah, Harakati ya Amal wala Muqawama wa Kitaifa, basi leo, kupitia “Makubaliano ya Mfumo”, wamebadilisha asili ya mapambano. Makubaliano haya yamegeuza vita kutoka katika mapambano ya kuwepo na makabiliano dhidi ya adui mtekaji, na kuvifanya kuwa jambo jingine.

Kuendelea kuwepo kwa adui Mzayuni katika ardhi yetu kunahusishwa na silaha za Muqawama

Alisema: Kwa mujibu wa dini zote za mbinguni na sheria za kimataifa, tuna haki ya kupigana na adui ili kumtoa katika ardhi yetu na kuishi kwa heshima, tatizo kuu la adui Mzayuni ni kwamba hajisikii kuwa salama isipokuwa baada ya kutuondolea silaha za Muqawama, na baada ya hapo, hatabaki na sababu yoyote ya kuwepo katika ardhi yetu.

Yaani, kuendelea kuwepo kwa adui Mzayuni katika ardhi yetu kunahusishwa na silaha za Muqawama; hii ndiyo sehemu hatari zaidi ya “Makubaliano ya Mfumo”, ingawa kuna vipengele vingine hatari pia.

Mjumbe wa Bunge la Lebanon alibainisha: Netanyahu amekuwa akisema mara kadhaa kwamba Wairani walijaribu kwa kila njia kututoa kusini mwa Lebanon, lakini mimi naishukuru Serikali ya Lebanon kwa makubaliano ambayo yanatuweka katika “Eneo la Njano.” Pia alirejelea kauli za Katz, Waziri wa Vita wa Israel, ambaye anaamini kwamba makubaliano na Lebanon yawatupatia haki ya kubaki katika ardhi ya Lebanon hadi pale silaha zitakapoondolewa; na hilo baada ya Iran kujaribu kuweka shinikizo kwa Marekani, kuilazimisha Israel kuondoka.

Sisi hatumwamini adui, na huenda akazungumza kwa namna hiyo ili kuzusha fitina baina yetu.

Kwa nini vipengele vya makubaliano haya vinafichwa?
Jashi alimuuliza Rais na Waziri Mkuu: Kwa nini vipengele vya makubaliano haya vinafichwa? Kwa nini Mwisraeli mmoja anasema kwa fahari na waziwazi: “Tumesaini makubaliano yenye manufaa kwa Israel”, na anafurahi, wakati sisi hatujapokea habari yoyote kutoka kwa Serikali au mamlaka za Lebanon kuhusu kile kilichosainiwa?

Kwa nini hamsemi ukweli? Ikiwa mnasema yana manufaa kwa Lebanon, basi tupeni maandishi yake, na jitokezeni kwenye televisheni mseme makubaliano haya yana manufaa gani kwa Lebanon? Hatuna nia ya kumtuhumu mtu yeyote, lakini ikiwa kweli yana manufaa kwa Lebanon, basi tuonyesheni ni kipengele gani kinachotunufaisha na mlisaini kwa msingi gani?

Alisisitiza kuwa: Mnajua kwamba “Makubaliano ya Mfumo” hayakuwasilishwa kwa Baraza la Mawaziri, kama chombo cha utendaji cha Lebanon, wala kwa Bunge la Wawakilishi. Kisingizio ni kwamba kwa kuwa haya ni makubaliano ya awali, hayahitaji kuwasilishwa bungeni; lakini kwa nini hata hayakuwasilishwa kwenye Baraza la Mawaziri? Na kwa nini kuna ufichaji huu?

Sisi tunasema hayana manufaa kwa Lebanon, nanyi mnasema yana manufaa; basi tuonesheni sababu yenu, sababu yetu ya kusema kwamba makubaliano haya hayana manufaa kwa Lebanon ni kwamba ndani yake adui wa Israel amepewa uhalali, na anachukua kila anachotaka; wakati uwepo wake leo nchini Lebanon umehalalishwa.

Makubaliano haya hata yamezuia watu kurejea katika nyumba zao; wakati hata Makubaliano ya Oslo hayakuzuia Wapalestina kurejea Palestina. Lakini makubaliano haya yanazuia watu kurejea na wanaambiwa: “Kurejea ni marufuku.”

Mjumbe wa Kambi ya Muqawama aliongeza: Baada ya raundi saba za mazungumzo yasiyo na maana, je, tumezuia kuendelea kwa mashambulizi ya adui? Je, tumemzuia adui kuwafukuza watu wetu kutoka katika nyumba zao kwa dhuluma na uchokozi katika eneo la Mansouri? Je, tumezuia milipuko na uharibifu? Je, raundi hizi saba za mazungumzo zimezuia milipuko?

Mlipuko mmoja ulikuwa sawa na tani 700 za vilipuzi, yaani sawa na mashambulizi 700 mazito ya anga; Waisraeli wenyewe wanasema: “Tulilipua tani 700 [za vilipuzi]”, bila kuhesabu milipuko mingine iliyotokea.

Aliendelea: Hata katika mmoja wa milipuko hiyo ambayo ilikuwa na nguvu ndogo zaidi, mtikisiko wenye nguvu ya daraja 3 kwa kipimo cha Richter ulihisiwa. Kwa hiyo, je, “Makubaliano ya Mfumo” haya yana manufaa kwa Lebanon?

Taifa letu linafahamu vizuri na linatofautisha kati ya kile ambacho kwa hakika kina manufaa kwao na wale wanaopanga njama dhidi yao na maslahi yao. Kwa hiyo, nguzo za madaraka zinazoshirikiana na Wamarekani na Waisraeli katika kuuangusha Muqawama na kuidhalilisha heshima ya taifa letu linalopambana, zinapaswa kufahamu wazi kwamba zitaanguka, na historia itaweka alama ya udhalili na kujisalimisha kwa adui wa Israel kwenye vipaji vya nyuso zao.

Taifa letu lenye fahari na heshima halikubali chochote isipokuwa kuishi kwa heshima

Jashi alisisitiza kwa kusema: Taifa letu lenye fahari na heshima halikubali chochote isipokuwa kuishi kwa heshima, tunawaheshimu baadhi ya washirika wetu wa kitaifa na tunakubali mitazamo yao; wao wanatukosoa na kusema: “Sisi tunataka tu kuishi.” Ni kweli, sisi na ninyi sote tunataka kuishi, lakini sisi tunataka kuishi kwa heshima.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha