Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, taasisi moja ya sanaa jijini London, chini ya paa la jengo la kale la Kihispania lenye historia ya takribani miaka 536, imeandaa maonesho ya sanaa yaliyochochewa na sanaa ya Kiislamu ya Mashariki ya London. Maonesho hayo yanaonesha mapazia matatu makubwa yaliyopambwa kwa michoro ya kisanii, ambayo yanaunganisha jamii za Kiislamu za jiji hilo na historia ndefu ya Waislamu barani Ulaya.
Miongoni mwa kazi za msanii mashuhuri, Shahid Salim, kuna michoro inayoonesha sera za uhasama za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uingereza mwaka 2013, pamoja na picha za wanunuzi Waislamu katika soko kubwa la Queens jijini London. Pia kuna picha ya Altab Ali, kijana wa Bangladeshi aliyeuawa katika bustani ya jiji hilo katika shambulio lililochochewa na ubaguzi wa rangi.
Bwana Salim, ambaye pia ni mbunifu wa majengo, mwandishi na mhadhiri wa chuo kikuu, alisema: Mkusanyiko huu wenye jina “Nilizaliwa Hapa”, unaelezea “hadithi ya uhamiaji na hali ya kuwa sehemu ya jamii.”
Aliongeza: Jumba la Makumbusho la Victoria and Albert liliniomba kuandaa maonesho ya sanaa katika sehemu ya mashariki ya jumba hilo, ambayo ina paa la kale lililochochewa na msikiti mmoja nchini Hispania.
Katika historia, “Ulaya ya Kikristo” imekuwa ikivutiwa na “mafanikio ya kisanii ya ustaarabu wa Kiislamu barani Ulaya”, na wakati mwingine imeyahifadhi na kuyatukuza. Hata hivyo, mara nyingi sera zisizo sahihi zimezisukuma jamii za Waislamu pembezoni, kuzitenga na kuzifanyia vitendo vya ukandamizaji na mateso.
Chanzo: Shirika la Habari la Al Jazeera
Maoni yako