Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Mwaliko huo umetolewa na Sheikh Abdulatif Swaleh, ambaye amewataka waumini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika hafla hiyo na kuitumia kama fursa ya kuongeza mapenzi kwa Mtume Muhammad (saww), kujifunza mafundisho yake na kuimarisha mshikamano na udugu miongoni mwa Waislamu.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hafla hiyo inatarajiwa kufanyika tarehe 1 Oktoba 2026, katika mtaa wa Stendi ya Zamani, Kondoa mjini, ambapo waumini kutoka Kondoa na maeneo ya jirani wanatarajiwa kushiriki katika tukio hilo la kiroho na kijamii.
Hafla hiyo pia inatarajiwa kuhudhuriwa na Masheikh mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania, akiwemo Sayyid Edarusi kutoka Lamu, pamoja na Sheikh Maulid kutoka Arusha, sambamba na Masheikh na wageni wengine ambao wanatarajiwa kushiriki katika kutoa nasaha na mafundisho mbalimbali katika hafla hiyo.
Waumini wote, familia na wapenda mafundisho ya Mtume (saww) wamehimizwa kutumia fursa hiyo kushiriki katika maadhimisho hayo kwa wingi, huku hafla hiyo ikitarajiwa kuwa sehemu muhimu ya kuhuisha mapenzi kwa Mtume (saww), kusambaza mafundisho yake na kuimarisha umoja wa Waislamu mjini Kondoa na Tanzania kwa ujumla.
Maoni yako