Jumapili 6 Septemba 2026 - 12:06
Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Yalikuwa Chanzo cha Hamasa kwa Wananchi wa Afrika Kusini

Hawza/ Naibu Rais wa Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu la Afrika Kusini, huku akisisitiza kwamba Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalikuwa chanzo cha hamasa kwa harakati za kupigania uhuru nchini Afrika Kusini baada ya kuonesha namna wananchi walivyoweza kusimama dhidi ya madola makubwa, amesema: Umoja wa mataifa hatimaye utaishinda dhulma na ubeberu.

Kwa mujibu wa Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Zafar Najjar, Naibu Rais wa Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu la Afrika Kusini, akizungumzia athari za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kwa mataifa yanayopigania uhuru duniani, amesema: Sisi wananchi wa Afrika Kusini, hususan baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran mwaka 1979 (1357 kwa kalenda ya Shamsi), tulijifunza mambo mengi kutoka katika mapinduzi hayo.

Aliendelea kusema: Mapinduzi ya Kiislamu yalituonesha kwamba nguvu za kijamii na matakwa ya wananchi vinaweza kusimama dhidi ya madola makubwa, na hata kuyapa changamoto madola ambayo yanaonekana kana kwamba hayawezi kushindwa.

Naibu Rais wa Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu la Afrika Kusini alisisitiza: Uzoefu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran uliithibitishia jamii ya kimataifa kwamba, bila kujali ukubwa wa nguvu zilizo upande wa pili, wananchi na jamii iliyoungana wanaweza kusimama imara dhidi yake.

Najjar alihitimisha kwa kusisitiza juu ya ushindi wa mkondo wa Muqawama dhidi ya dhulma na ubeberu, akasema: Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na kwa umoja wa Waislamu, kambi ya dhulma na uistikbari itashindwa, na mataifa ya Kiislamu pamoja na mataifa yanayopigania uhuru duniani, kwa kutegemea imani na umoja, yataweza kuunda mustakabali tofauti.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha