Jumatatu 7 Septemba 2026 - 10:14
Hadithi ya Leo | Madhara Yanayopatikana Kutokana na Kuipenda Dunia

Hawza/ Imam Musa Al-Kadhim (as), katika riwaya, anaeleza kuhusu kutotosheka mwanadamu katika kuifuata dunia, pamoja na umuhimu wa kujiepusha na kushikamana nayo kupita kiasi.

Shirika la Habari la Hawza, linachapisha riwaya ifuatayo kutoka katika kitabu “Tuhaf al-Uqul”.

Imam Musa Al-Kadhim (as) amesema:

«مَثَلُ الدُّنْیَا مَثَلُ مَاءِ الْبَحْرِ، کُلَّمَا شَرِبَ مِنْهُ الْعَطْشَانُ ازْدَادَ عَطَشًا حَتَّی یَقْتُلَهُ.»

“Mfano wa dunia ni kama maji ya bahari; kila mwenye kiu anapokunywa kutoka humo, kiu yake huongezeka zaidi, mpaka hatimaye maji hayo yanamuangamiza.”

Maana ya hadithi hii ni kwamba dunia, mali zake, mapambo yake na starehe zake ni sawa na maji ya bahari. Mwanadamu mwenye kiu akinywa maji ya bahari, badala ya kiu chake kumalizika, huongezeka zaidi, na huendelea kunywa mpaka maji hayo yanapomwangamiza.

Hadithi hii inatufahamisha kwamba; tamaa ya kupindukia ya mali na starehe za dunia haina kikomo. Kadiri mwanadamu anavyomiliki na kutafuta zaidi bila kuridhika, ndivyo tamaa yake inavyozidi kuongezeka, na ikiwa hatajiwekea mipaka, tamaa hiyo inaweza hatimaye kuwa sababu ya kumuangamiza.

Chanzo: Tuhaf al-Uqul, uk. 396.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha