Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, wajumbe wa Bodi ya Elimu na Malezi katika Jimbo la Texas wameidhinisha uandishi mpya wa maudhui ya masomo ya shule za sekondari za Texas katika somo la Masomo ya Jamii, huku wakipuuza maombi ya Waislamu waliokuwa wakisisitiza kwamba shule zinapaswa kuwafundisha wanafunzi jinsi Waislamu walivyochangia katika historia ya dunia.
Watu wenye chuki dhidi ya Uislamu, pamoja na wengine wengi wa chama cha Republican, badala ya kuzingatia shughuli za kibinadamu zilizofanywa na Waislamu, wamepitisha somo ambalo, kwa mfano, linawalazimisha wanafunzi wa shule kujifunza kwamba “Uislamu ni dhehebu lisilo la Kimungu” na kwamba ulikuwa msukumo mkuu wa mashambulizi ya Septemba 11, badala ya kuelekeza mjadala katika makundi ya kigaidi kama vile Al-Qaeda na watu wenye misimamo mikali kama Osama bin Laden.
Lakini ukweli ni kwamba hata mtaalamu Muislamu wa Marekani wa huduma za dharura za kitabibu alikuwa miongoni mwa watu waliouawa wakati akijaribu kuokoa maisha ya watu katika kipindi cha janga hilo. Hata hivyo, kwa masikitiko, msisitizo mdogo umetolewa kuhusu mambo haya.
Bodi ya Elimu na Malezi ya Texas, kwa kushirikiana na Wafuasi wa jamhuri ya kisekula duniani, inakusudia kuutambulisha Uislamu kama dini isiyo ya Kimungu na inayopinga ubinadamu. Hii ni licha ya ukweli kwamba kila mtu anajua kuwa madai haya hayana msingi sahihi, na kwamba kuyatumia katika vitabu vya kiada ni dhuluma iliyo wazi dhidi ya jamii.
Chanzo: cbsaustin.com
Maoni yako