-
Hadithi ya leo:
DiniUsiache wajibu hizi mbili kubwa za Mwenyezi Mungu
Kwa hakika kuamrisha mema na kukataza maovu ni faradhi mbili kubwa, kwazo faradhi husimamishwa.
-
Hadithi ya leo:
DiniKuwa hivi katika maingiliano na watu
Ingilianeni na watu kwa namna ambayo mkifa wakulilieni, na mkiwa hai (na ikawa hawajakuoneni kwa muda) wawe na shauku ya kukuoneni.
-
Hadithi ya leo:
DiniLipe uzito suala la haki za watu
Mwenye kula mali ya nduguye kwa dhulma na asimrudishie mwenyewe, basi chakula chake Siku ya Kiyama ni miali ya moto.
-
Hadithi ya leo:
DiniUsicheleweshe kulipa ujira wa kibarua
Mlipe kibarua kabla jasho lake halijakauka.
-
Hadithi ya leo:
DiniSema haki, kwani kuokoka kwako kuko katika hilo
Mche (muogope) Mwenyezi Mungu na sema haki hata kama utaangamia, kwani (kwa hakika) kuokoka kwako kuko katika hilo. Mche Mwenyezi Mungu na acha batili hata kama kuokoka kwako kuko katika hilo,…
-
Hadithi ya leo:
DiniUsipuuze sauti ya wengine ya kuomba msaada
Mwenye kusikia sauti ya mwenye kuomba msaada na asiende kumsaidia, huyo sio Muislamu.
-
Hadithi ya leo:
DiniKatu usifanye khiana katika amana
Mcheni Mwenyezi Mungu na rudisheni amana kwa yule aliyekuaminini.
-
Hadithi ya leo:
DiniNi wajibu kwako kuchunga haki za kila mtu (awe Muislamu au sio Muislamu)
Kuna makundi mawili ya watu: Ama ni ndugu yako katika dini, au anayefanana na wewe katika uumbaji; kwa hali yoyote, unapaswa kuheshimu haki zao.
-
Hadithi ya leo:
DiniChunga (mazingira) asili
Itakapowadia Siku ya Kiyama na mmoja wenu akawa ana mche mkononi mwake, akiweza kuupanda kabla ya kusimama Kiyama, basi aupande.
-
Hadithi ya leo:
DiniChunga haki za wanyama
Kila unapowakabidhi wanyama kwa mtu mwaminifu, muagizie asitengananishe kati ya ngamia na mtoto wake, na asikamue maziwa yake kiasi cha kumdhuru mtoto... .
-
Hadithi ya leo:
DiniKuwa hivi kwa watu
Kuwa mlaini kwa watu, kuwa na maneno mazuri na kutana na ndugu yako kwa bashasha na tabasamu.
-
Hadithi ya leo:
DiniJipambe kwa tabia njema
Tabia njema ni; Kumsamehe aliyekudhulumu, kuunga udugu aliyekukatia (udugu), kumpa aliyekunyima na kusema haki hata kama ni kwa madhara yako.
-
Hadithi ya leo:
DiniKuwa mtu wa utani (mzaha), lakini chunga mpaka wake
Mwenyezi Mungu anampenda afanyae mzaha katika mkusanyiko, kwa sharti asitukane na kutoa maneno machafu.
-
Hadithi ya leo:
DiniKuwa hivi katika biashara
Yeyote anayefanya biashara (anauza na kununua) lazima aepuke vitu vitano, kinyume na hivyo asinunue au kuuza kabisa: Riba, kuapa, kuficha ubovu (wa bidhaa), kusifu bidhaa anazouza, na kukashifu…
-
Hadithi ya leo:
DiniUombezi wa mwanamke mbele ya Mwenyezi Mungu
Hakuna uombezi wa mwanamke mbele ya Mwenyezi Mungu wenye kuokoa zaidi kama radhi ya mumewe. (mumewe kuwa radhi naye)
-
Hadithi ya leo:
DiniLipe uzito suala la heshima na ridhaa ya mwenza
Hakika aliye mbora zaidi miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule ambaye anamheshimu zaidi mwenza wake.
-
Hadithi ya leo:
DiniWeka mambo yako katika mkondo wa haki
Hakuacha haki mwenye izza (heshima) isipokuwa alidhalilishwa, na dhalili hakuchukua haki isipokuwa alipata izza (heshima).
-
Hadithi ya leo:
DiniDaima kuwa mtu huru
Usiwe mtumwa wa mwingine, ilihali Mwenyezi Mungu amekuumba ukiwa huru.
-
Hadithi ya leo:
DiniJiepushe na talaka
Oeni wala msitaliki, kwani hakika talaka inatikisha arshi ya Mwenyezi Mungu.
-
Hadithi ya leo:
DiniIfundishe familia yako maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu
Katika kauli yake Mwenyezi Mungu alotukuka utajo wake" Jiokoeni nafsi zenu na familia zenu na moto".
-
Hadithi ya leo:
DiniWeka kando tabia ya kujiona
Kujiona (kujikweza) kunamkwaza mtu kutafuta elimu na kunaleta udhalili na ujahil.
-
Hadithi ya leo:
DiniChunga vitendo vyako
Tambua kwamba, hautasalimika katu na jicho la Allah, basi tazama jinsi unavyotenda.
-
Hadithi ya leo:
DiniOgopa kilio na laana ya aliyedhulumiwa
Ogopa kilio na laana ya aliyedhulumiwa (madhulumu), hata akiwa kafiri, kwa sababu hakuna kizuizi dhidi ya laana ya aliyedhulumiwa.
-
Hadithi ya leo:
DiniKwa kumfurahisha mwanao, mfurahishe pia Mwenyezi Mungu
Mwenye kumfundisha mtoto wake Qur'an, basi mtoto huyo ataitwa [Siku ya Kiyama] pamoja na wazazi wake na kuwavisha mavazi mawili ambapo nyuso za watu wa peponi zitang'aa kutokana na nuru yao.
-
Hadithi ya leo:
DiniChunguza dafina (hazina) za Qur'ani
Aya za Qur'an ni dafina (hazina), na hazina inapofunguliwa, unapaswa kuona kilichomo ndani yake.
-
Hadithi ya leo:
DiniTanguliza utakasifu (kujiheshimu) katika kuamiliana na asiyekuwa maharimu
Kuweni na utakasifu (jiheshimuni) kwa wanawake wa watu, ili wanawake wenu wafanyiwe utakasifu (waheshimiwe).
-
Hadithi ya leo:
DiniTambua haki za watu na uzitekeleze
Daraja (cheo) ya juu mbele ya Mwenyezi Mungu ni ya mtu anayetambua haki za watu na akafanya juhudi zote kutimiza haki zao.
-
Hadithi ya leo:
DiniAcha maisha ya kidhalili
Kifo cha heshima ni bora kuliko maisha ya kidhalili. Mauti ni bora kuliko kuhusishwa na udhalili, na udhalili ni bora kuliko kuingia Motoni.
-
Hadithi ya leo:
DiniKuwa katika orodha ya waja wema kabisa wa Mwenyezi Mungu
Ni wale ambao wanapofanya jema hufurahi, watendapo (jambo) baya huomba maghufira, wakipewa kitu hushukuru, na wakifikwa na majaribu (mtihani) huonyesha subira na wanapokasirika husamehe.
-
Hadithi ya leo:
DiniKuwa hivi wakati wa hasira, wa kuridhia na kuwa na nguvu
Muumini anapokasirika, hasira yake haimuondoi katika haki.