Alhamisi 13 Machi 2025 - 14:00
Chunga haki za wanyama

Kila unapowakabidhi wanyama kwa mtu mwaminifu, muagizie asitengananishe kati ya ngamia na mtoto wake, na asikamue maziwa yake kiasi cha kumdhuru mtoto... .

Shirika la Habari la Hawza - Imamu Ali (a.s) alibainisha namna ya kuamiliana na wanyama ambao walitolewa kama Zaka:

«... فَإِذَا أَخَذَهَا أَمِينُكَ فَأَوْعِزْ إِلَيْهِ أَلَّا يَحُولَ بَيْنَ نَاقَةٍ وَ بَيْنَ فَصِيلِهَا وَ لَا يَمْصُرَ لَبَنَهَا فَيَضُرَّ [فَيُضِرَّ] ذَلِكَ بِوَلَدِهَا وَ لَا يَجْهَدَنَّهَا رُكُوباً وَ لْيَعْدِلْ بَيْنَ صَوَاحِبَاتِهَا فِي ذَلِكَ وَ بَيْنَهَا، وَ لْيُرَفِّهْ عَلَى اللَّاغِبِ وَ لْيَسْتَأْنِ بِالنَّقِبِ وَ الظَّالِعِ وَ لْيُورِدْهَا مَا تَمُرُّ بِهِ مِنَ الْغُدُرِ وَ لَا يَعْدِلْ بِهَا عَنْ نَبْتِ الْأَرْضِ إِلَى جَوَادِّ الطُّرُقِ وَ لْيُرَوِّحْهَا فِي السَّاعَاتِ وَ لْيُمْهِلْهَا عِنْدَ النِّطَافِ وَ الْأَعْشَابِ... .»

Kila unapowakabidhi wanyama kwa mtu mwaminifu, muagizie asitengananishe kati ya ngamia na mtoto wake, na asikamue maziwa yake kiasi cha kumdhuru mtoto. Wakati wa kupanda ngamia chunga uadilifu, zingatia hali ya ngamia aliyechoka au aliyejeruhiwa ambapo ni vigumu kumfanya kipango. Awachukue na kuwapeleka sehemu za maji, na wala asiwatoe kwenye njia zenye nyasi pande zote mbili hadi kwenye njia isiyo na majani, na kila mara awape ngamia muda wa kupumzika, na kila wanapofika kwenye maji na majani, awape muda wa kula nyasi na kunywa maji."

Nahaj al-Balagha, barua ya 25

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha