Jumatano 18 Februari 2026 - 00:56
Hatari zaidi kuliko Manowari ni silaha inayoweza kuizamisha hiyo Manowari hadi kwenye kina cha bahari

Hawza/ Kiongozi Mkuu, katika kujibu vitisho vya Marekani, amesema: Hatari kuliko manowari ni silaha inayoweza kuipeleka hadi kina cha bahari.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, asubuhi ya jumanne katika mkutano uliokuwa na shauku kubwa uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Tabriz na jimbo la Azarbaijan Mashariki, ameuita mwaka huu kuwa ni mwaka wa ajabu na wenye matukio mengi, na akataja “ushindi wa taifa katika vita vya siku 12”, “kuzimwa kwa fitna kubwa na nzito ya mwezi wa Dey” na “ushiriki wa kishindo wa wananchi katika maandamano mawili makubwa ya tarehe 22 Dey na 22 Bahman” kuwa ni alama za nguvu na uhai wa taifa tukufu la Iran. Akitilia mkazo juu ya kuhifadhi na kuimarisha “utayari, umakini na umoja wa kitaifa”, aliongeza: Isipokuwa vinara na vipengele vya uharibifu vilivyounganishwa na maadui, mashahidi na waliopoteza maisha katika machafuko, wawe ni “vikosi vya kulinda usalama na utulivu wa jamii”, “wapita njia wasio na hatia” au hata “waliodanganyika ambao kwa sababu ya wepesi na hasira waliandamana na fitna”, wote tunawaona kuwa ni watoto wetu, na sisi tuna huzuni na maombolezo kwa ajili ya wote hao.

Mtukufu Ayatollah Ali Khamenei alisisitiza juhudi maradufu za viongozi wa serikali katika kutatua matatizo, kudhibiti mfumuko wa bei na kuhifadhi thamani ya sarafu ya taifa. Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, akirejea uingiliaji usiofaa na vitisho vya kiburi vya maafisa na vyombo vya habari vya Marekani kuhusu kuishambulia Iran, alisema: Wao wenyewe wanajua kuwa hawana uwezo wa kustahimili maneno na matendo hayo, na “jeshi linalojiona kuwa ndilo lenye nguvu zaidi duniani” linaweza kupigwa kofi kali kiasi kwamba lishindwe kusimama tena; huku akibainisha kuwa vyombo vinavyohusika na kukabiliana na vitisho vina utayari unaohitajika, na wananchi wanapaswa kuendelea na kazi na maisha yao kwa utulivu na kujiamini.

Katika mkutano huo uliofanyika katika mkesha wa kumbukumbu ya harakati ya kihistoria na yenye maamuzi ya tarehe 29 Bahman 1356 ya wananchi wa Tabriz, alisema “kujua wakati sahihi, kuchukua hatua kwa wakati na kujitolea” kuwa ni miongoni mwa sifa za harakati hiyo. Akikisifu pia kizazi kipya cha Azarbaijan kwa uwepo wao wenye matumaini katika nyanja mbalimbali, alisema: Kuongezeka maradufu kwa ushiriki wa watu wa Tabriz katika maandamano ya 22 Bahman kulithibitisha kwamba wao, kama taifa zima la Iran, wako hai na wenye nguvu; na taifa la namna hii halidanganyiki na michezo ya kisiasa na hila za adui.

Kiongozi wa Mapinduzi alieleza kuwa, mwaka huu ni mwaka wa kufunuliwa mara kadhaa kwa “utukufu, irada, azma thabiti na uwezo mwingine wa taifa la Iran”, na akaongeza: Taifa kwa kuonyesha nguvu mara kwa mara na kusimama kidete, limeifanya Iran kuwa na heshima na utukufu; na maafisa wanaosafiri nje ya nchi katika siku hizi, wanahisi vyema upekee wa taifa hili wanapokutana na viongozi wa nchi nyingine.

Alisisitiza umuhimu wa kufafanuliwa kwa undani wa fitna ya mwezi wa Dey kupitia “watu wa fikra na uchambuzi”, akisema: Kilichotokea hakikuwa tu harakati na machafuko ya vijana na wasio vijana waliokasirika, bali yalikuwa ni “mapinduzi ya kijeshi yaliyopangwa” ambayo yalikanyagwa chini ya miguu ya taifa la Iran.

Katika kufafanua ukweli huo, aliongeza: Vyombo vya kijasusi vya Marekani na utawala wa Kizayuni, kwa msaada wa baadhi ya vyombo vya kijasusi vya nchi nyingine, tangu zamani vilivutia watu waovu au wenye mwelekeo wa uovu, vikawapa mafunzo, fedha na silaha nje ya nchi, na kuwatuma ndani kwa ajili ya kufanya hujuma na mashambulizi dhidi ya vituo vya kijeshi na vya serikali ili waingie uwanjani katika fursa mwafaka; na fursa hiyo waliipata katikati ya mwezi wa Dey.

Akirejea mazingira ya vitisho katika propaganda na kauli za maafisa wa Marekani na vyombo vya habari vya Kizayuni vinavyofanya kazi Marekani dhidi ya nchi yao, alisema: Ninyi watu wa Tabriz na taifa la Iran mlitoa jibu la vitisho na maneno yao yasiyo na maana siku ya 22 Bahman, na mkadhihirisha kwamba, vitisho si tu havina athari bali huongeza ari ya taifa.

Alisisitiza kuwa; licha ya vitisho vya vita, Wamarekani wanajua kuwa kutokana na matatizo yao ya kisiasa, kiuchumi na hadhi ya kimataifa, hawana uwezo wa kustahimili matokeo yake; na wanajua wakifanya kosa, mustakabali gani unawangoja.

Alitaja miongoni mwa ishara nyingine za kudorora kwa himaya ya kifisadi na dhalimu ya Marekani kuwa ni kukosa kwao mantiki, akisema: Mfano wa kukosa mantiki ni uingiliaji wao katika masuala ya Iran, miongoni mwake suala la silaha.

Alisema; umiliki wa silaha za kujihami ni jambo la lazima; kwani nchi yoyote bila silaha za kujihami hukanyagwa na maadui. Hata hivyo Wamarekani wanaingilia na kusema msipate aina fulani au masafa fulani ya makombora; ilhali hilo ni suala la taifa la Iran na halihusiani nao.

Alitaja pia uingiliaji wa Marekani katika haki ya Iran ya kumiliki teknolojia ya nyuklia ya amani kwa ajili ya uendeshaji wa nchi, tiba, kilimo na nishati kuwa ni ukosefu mwingine wa mantiki, akisema: Hili ni jambo la taifa la Iran; linawahusu nini nyinyi?

Akiashiria kauli mbiu ya wananchi kwamba “nishati ya nyuklia ni haki yetu ya kimsingi”, alisema: Haki ya kumiliki mitambo ya nyuklia na kurutubisha imekubaliwa katika mikataba na kanuni za Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki; na uingiliaji wa Wamarekani katika haki za kitaifa unaonyesha fikra zisizo na mpangilio za viongozi wao wa leo na jana.

Alisema; ukosefu wa mantiki wa ajabu zaidi ni namna wanavyotualika katika mazungumzo, wakisema: Njooni tuzungumze kuhusu nishati ya nyuklia, lakini matokeo yake yawe kwamba ninyi msiwe nayo!

Alisisitiza kuwa; kama mazungumzo yatafanyika, kuweka matokeo yake kabla ni kosa na upumbavu; na akasema; serikali rais na baadhi ya maseneta wa Marekani wanafanya upumbavu huo bila kutambua kuwa ni njia ya kufikia kikomo.

Akiashiria vitisho vya mara kwa mara vya Rais wa Marekani kuhusu kuwa na jeshi lenye nguvu zaidi duniani, alisisitiza: Hata jeshi lenye nguvu zaidi duniani wakati mwingine linaweza kupigwa kofi kiasi kwamba lishindwe kusimama.

Kuhusu hatua nyingine ya Marekani ya kutuma manowari kuelekea Iran, alisema: Manowari ni chombo hatari, lakini hatari zaidi ni silaha inayoweza kuizamisha hadi kina cha bahari.

Akiashiria kukiri kwa Rais wa Marekani kwamba wameshindwa kuiangamiza Jamhuri ya Kiislamu licha ya kupita miaka 47 tangu Mapinduzi, alisisitiza: Huku ni kukiri kuzuri; na mimi nasema hata hutoweza kufanya hivyo, kwa kuwa Jamhuri ya Kiislamu si serikali iliyotenganishwa na watu, bali inategemea taifa lililo hai, thabiti na imara ambalo katika miaka hii 47 limefanya kazi na juhudi kwa ajili ya maendeleo yake.

Aliongeza kuwa; kama adui alishindwa kung’oa mche mdogo wa Jamhuri ya Kiislamu katika siku za mwanzo za Mapinduzi, leo kwa rehema za Mwenyezi Mungu, umekuwa ni mti uliobarikiwa, mrefu na wenye matunda mengi, na nchi yenye uwezo mwingi; na maafisa wa serikali wanapaswa kutumia uwezo huo kuongeza juhudi zao ili kurekebisha mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya sarafu ya taifa, ambavyo vyote ni visivyo na mantiki, na kwa matumaini ya Mwenyezi Mungu vitarekebishwa.

Aliashiria kuendeleza umakini kwa kuzingatia pande zote, kwa kazi zilizoanza, kuondoa matatizo na kutuliza mazingira ya biashara kuwa ni wajibu wa maafisa, na akasema: Ikiwa kuna vitisho, pia kuna vyombo vya kuvizima; kwa hiyo wananchi waendelee bila wasiwasi na kazi, maisha, masomo, biashara na shughuli zao.

Alisisitiza umuhimu wa utulivu na kujiamini kutawala nchini, na akamuomba Mwenyezi Mungu ateremshe utulivu na faraja katika nyoyo za wananchi na awajaalie maafisa mafanikio katika kutekeleza majukumu yao.

Alisema pia “kuathiri na kuwachochea hasira baadhi ya wasio na uzoefu na wepesi” kuwa ni hatua nyingine ya waamrishaji na watekelezaji wa fitna, akielezea: Vipengele vilivyopata mafunzo viliwasukuma watu hao mbele, na wao wenyewe kwa silaha mbalimbali na sera ya “hatua kali na isiyo na kujali” waliingia uwanjani na kama kundi la kigaidi la Islamic State (Daesh), kwa ukatili wa ajabu “walichoma moto, waliua na kuharibu”.

Alisema, lengo kuu la vitendo hivyo lilikuwa kuyumbisha misingi ya mfumo, lakini vikosi vya polisi, Basij, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi na wananchi wengi walisimama dhidi ya wachochezi wa machafuko, na “mapinduzi ya kijeshi” hayo, licha ya maandalizi na gharama kubwa, yalishindwa waziwazi, na taifa likawa mshindi.

Alieleza kuwa “maandamano ya ajabu ya 22 Dey na 22 Bahman” ni miongoni mwa “alama za Mwenyezi Mungu”, na akasisitiza: Taifa hili tukufu lililoweza kushinda maovu na njama za adui kwa namna hii, linapaswa kwa “utayari, umakini na umoja wa kitaifa” kuhifadhi mafanikio haya ya wazi ya Mwenyezi Mungu.

Kuhusu damu zilizomwagika katika machafuko, alisema: Baadhi ya vinara wa fitna na waliokuwa sehemu ya mapinduzi hayo walipata adhabu yao, na hesabu yao iko kwa Mwenyezi Mungu; lakini makundi matatu mengine ya waliopoteza maisha, tunawaona kuwa ni watoto wetu na tunaomboleza kwa ajili yao wote.

Aliyataja makundi hayo kuwa ni: Kundi la kwanza, yaani “vikosi vya polisi, Basij, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi na wananchi waliokuwa pamoja nao” kuwa ni mashahidi wa juu wa usalama na utulivu wa jamii na mfumo. Kundi la pili ni “wapita njia na wananchi wasio na hatia” ambao pia ni mashahidi kwa kuwa waliuawa katika fitna iliyochochewa na adui. Na kundi la tatu ni “waliodanganyika kwa sababu ya wepesi wao na wakaandamana na wachochezi wa fitna”; nao pia ni sehemu yetu na watoto wetu, na tuna huzuni kwa ajili yao na tunamuomba Mwenyezi Mungu awarehemu na kuwaghufiria wote waliopoteza maisha.

Aliongeza kuwa, baadhi ya waliodanganyika ambao hawakukamatwa wala kufungwa, wamemwandikia barua wakionesha kujuta na kuomba msamaha.

Akiashiria kukiri kwa Wamarekani kuunda Daesh, alisema: Daesh ile kwa kiasi fulani imeangamizwa, lakini hawa ni “Daesh wapya”, na katika suala hili maafisa na wananchi wote wanapaswa kuwa macho, hususan vijana wawe waangalifu kujua nani anawaambia nini na anawapa mapendekezo gani.

Kiongozi wa Mapinduzi alisisitiza kuwa, wananchi wanataka viongozi wakuu wa machafuko wafuatiliwe na kuadhibiwa, na vyombo vya mahakama na usalama vina wajibu wa kuwafikisha mahakamani na kuwaadhibu; na kwa wale wanaoandamana na adui “kwa maneno, uchambuzi au vitendo”, wachukuliwe hatua za kisheria kwa uadilifu.

Aliongeza: Inawezekana sana mpango ujao wa Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ukawa wa mtindo huu huu; lakini bila shaka, kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na kwa sababu ya utayari na uhai wa taifa, harakati yoyote ya aina hiyo itazimwa kwa msimamo thabiti wa taifa.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, alitaja matatizo mengi ya kiuchumi, kisiasa na kijamii ya Marekani kuwa ni ishara za mchakato wa kudorora na kutoweka kwa himaya ya Marekani, akisema: Tatizo la Marekani nasi ni kwamba inataka kuimeza Iran, lakini taifa la Iran na Jamhuri ya Kiislamu vinazuia kutimia kwa lengo lao.

Alisema; maneno ya vitisho ya Rais wa Marekani yanaonyesha tamanio lao la kulitawala taifa la Iran, na akaongeza: Taifa la Iran linayajua vyema mafundisho yake ya Kiislamu na Kishia, na linajua ni wakati gani na lipi linapaswa kufanya.

Akiashiria kauli ya kihistoria ya Husseinn ibn Ali kwamba; mtu kama mimi hawezi kumpa kiapo cha utiifu mtu kama Yazid, alibainisha: Taifa la Iran pia linasema kuwa taifa kama sisi, lenye utamaduni, historia na maarifa ya hali ya juu, haliwezi kutoa kiapo cha utiifu kwa watu mafisadi wanaotawala Marekani.

Alisema; kufichuka kwa ufisadi wa kushangaza katika kisa cha “kisiwa” kunaonesha uhalisia wa ustaarabu na demokrasia ya kiliberali ya Magharibi; na kwamba huu ni mfano tu wa maovu yao mengi, na kama hili lilivyokuwa limefichwa kisha likafichuka, mengine mengi pia yatafichuka baadaye.

Kabla ya hotuba ya Kiongozi wa Mapinduzi, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Motahhari Asl, Mwakilishi wa Wali al-Faqih katika jimbo la Azarbaijan Mashariki na Imamu wa Ijumaa wa Tabriz, huku akirejea msimamo thabiti wa vikosi vya kijeshi na wananchi wa jimbo hilo mbele ya vita vya kulazimishwa vya utawala wa Kizayuni na ushiriki mkubwa katika matembezi ya tarehe 22 Dey na 22 Bahman, alisema: Wananchi wa Azarbaijan daima wako uwanjani kutekeleza majukumu yao yote ya Kiislamu, kimapinduzi na kitaifa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha