Alhamisi 19 Februari 2026 - 00:30
Mradi mkubwa zaidi wa upanuzi wa Haram ya Imamu Hussein (as) wenye ukubwa wa mita za mraba 330,000 waanza

Hawza/ Idara ya miradi ya maendeleo ya Ataba Tukufu ya Husseini imetangaza sifa za mradi wa uwanja wa Sahn Rasul A’dham (Swalla-Llahu alayhi wa Aalihi wa sallam).

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, idara ya miradi ya maendeleo ya Ataba Tukufu ya Husseini imetangaza maelezo na sifa za mradi wa Sahn Rasul A’dham (Swalla-Llahu alayhi wa Aalihi wa sallam); mradi ambao unahesabiwa kuwa ni hatua ya tatu ya mpango mkubwa wa upanuzi wa uwanja wa Haram ya Haram ya Imamu Hussein, na hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi iliyofanyika siku ya Jumatano, tarehe 18 Februari 2026, (29 Shaban 1447)

Mhandisi Hussein Ridha Mahdi, mkuu wa idara hiyo, alisema: Eneo la ujenzi wa mradi wa Sahn Rasul A’dham (Swalla-Llahu alayhi wa Aalihi wa sallam) ni mita za mraba 330,000, huku eneo lote la ardhi yake likiwa mita za mraba 100,000; kwa hiyo, mradi huu utakuwa miongoni mwa miradi mikubwa ya ujenzi ambayo itachukua nafasi muhimu katika kupokea idadi kubwa ya mazuwari.

Akifafanua kwamba mradi wa Sahn Rasul A’dham (Swalla-Llahu alayhi wa Aalihi wa sallam) unaunda hatua ya tatu ya mpango mkubwa wa upanuzi wa uwanja wa Imamu Hussein (as), aliongeza: Uwanja huu unahesabiwa kuwa mradi mkubwa zaidi wa maendeleo katika historia ya uwanja mtukufu wa Husseini.

Mahdi aliendelea kusema: Eneo la utekelezaji wa mradi litakuwa upande wa kaskazini-magharibi wa uwanja mtukufu wa Husseini, na umeundwa katika mfumo wa dira ya kihandisi ya kina yenye lengo la kuendeleza miundombinu na kupanua maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kuwahudumia mazuwari.

Pia alieleza kwamba; hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi wa mradi itafanyika Jumatano, tarehe 18 Februari 2026, ili kutangaza rasmi kuanza kwa hatua mpya ya utekelezaji wa upanuzi huo.

Mpango wa upanuzi wa uwanja wa Imamu Hussein (as) ni miongoni mwa miradi mikubwa ya ujenzi inayotekelezwa na Ataba Tukufu ya Husseini kwa lengo la kupokea idadi inayoongezeka ya mazuwari na kuandaa mazingira yanayofaa kwa ajili ya ziara pamoja na huduma za kidini na kijamii.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha