Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, video iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii inaonyesha wanaume Waislamu waliokuwa wakishiriki maandamano nje ya Ukumbi wa Jiji la Sydney wakiwa katika swala ya jamaa.
Mmoja wa waliorekodiwa katika video hiyo alitupwa chini na polisi. Mtu huyo anaitwa Shahbaz Jamal, na katika mahojiano amesema kuwa; waandamanaji hao walichagua kwa makusudi eneo la kuswalia kabla ya kuanza swala, mbali na polisi, magari na wapita-njia, ili kuepusha kutokea kwa sintofahamu. Pia baadhi yao waliunda duara la ulinzi kuwazunguka wanaoswali, lakini polisi bado walifika kwa vitisho.
Watu waliokuwa wakiwazunguka wanaoswali waliwaeleza polisi kwamba hiyo ilikuwa ni swala ya jamaa tu na dua ya pamoja, lakini polisi waliendelea kuwatupa wanaoswali. Kwanza waliwatishia waliokuwa katika safu za nyuma — ambao walikuwa wanawake — na kuwatawanya, kisha wakawafikia wengine na kuwatupa mmoja baada ya mwingine kana kwamba ni taka. Amesema hakutarajia kuona tabia ya kikatili kama hiyo mjini Sydney.

Shirika la Haki za binadam katika taarifa yake jioni ya Jumanne liliandika kuwa, serikali ya New South Wales inapaswa kuchunguza matumizi ya nguvu kupita kiasi yaliyotumiwa na polisi, na kuwachukulia hatua stahiki wale waliohusika, ikiwa ni pamoja na kuwaadhibu au kuwafikisha mahakamani.
Chanzo: SBS
Maoni yako