Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Khamenei ametoa jibu kwa istifta hiyo kuhusu “kusahau nia ya kufunga,” ambalo linawasilishwa kwenj kama ifuatavyo:
Kusahau nia ya kufunga
Swali:
Ikiwa mtu alikuwa tayari na uamuzi wa hakika tangu awali wa kufunga siku maalumu — kama siku ya Dahwal-Ardh — lakini akasahau, na siku hiyo akala chakula au akanywa maji, kisha akakumbuka, je! Hukumu ya funga yake ya siku hiyo ni ipi?
Jibu:
Ikiwa alikuwa ameweka nia ya kufunga tangu usiku uliotangulia kwa ajili ya kesho, funga yake ni sahihi. Lakini kama alikuwa amesahau na hakuweka nia, na alikuwa tu na azma ya jumla ya kufunga tangu siku zilizopita, hilo halitoshi.
Maoni yako