Shirika la Habari la Hawza - Mtume (s.a.w.w) aliulizwa kuhusiana na waja wema kabisa wa Mwenyezi Mungu. Akasema:
«اَلَّذِينَ إِذَا أَحْسَنُوا اِسْتَبْشَرُوا وَ إِذَا أَسَاءُوا اِسْتَغْفَرُوا وَ إِذَا أُعْطُوا شَكَرُوا وَ إِذَا اُبْتُلُوا صَبَرُوا وَ إِذَا غَضِبُوا غَفَرُوا.»
Ni wale ambao wanapofanya jema hufurahi, watendapo (jambo) baya huomba maghufira, wakipewa kitu hushukuru, na wakifikwa na majaribu (mtihani) huonyesha subira na wanapokasirika husamehe.
Wasail al-Shiah, Jz 16, uk 67
Maoni yako