Ijumaa 30 Oktoba 2026 - 01:00
Maandamano ya Maombolezo ya Kifo cha Kishahidi cha Bibi Fatima Zahra (sa) Chini ya Vitisho vya Usalama

Hawza/ Licha ya hali kali ya kiusalama na vitisho vinavyoendelea kutolewa na utawala wa Bahrain wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi kwa Bibi Fatima Zahra (sa), misafara ya waombolezaji ilipita katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Hatua hiyo ililenga kusisitiza msimamo wa wananchi wa kushikamana na utambulisho wao wa kidini na kudumisha alama na desturi za kidini za Ahlul-Bayt (amani iwe juu yao).

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, wananchi wa Bahrain hawakujali kabisa hali kali ya tahadhari ya kiusalama iliyokuwa imetangazwa katika baadhi ya maeneo, hususan katika barabara ya Al-Budaiya, wakati wa siku za kuadhimisha kumbukumbu ya kuuawa kishahidi Bibi Fatima Zahra (amani iwe juu yake).

Kinyume na kuimarishwa hatua za kiusalama na vitisho vilivyokuwa vikitolewa mfululizo, misafara ya waombolezaji ilijitokeza katika mitaa ya miji mingi ya Bahrain ili kuthibitisha uaminifu na mshikamano wao katika kudumisha alama na desturi za kidini, pamoja na kuendeleza kumbukumbu na kutaja majina ya Ahlul-Bayt (amani iwe juu yao).

Sambamba na hayo, huku wito wa kuitisha “Siku ya Hasira ya Wananchi, tarehe 8 Novemba” ukizidi kushika kasi, harakati ya mapinduzi ya wananchi inaendelea kusisitiza kwa nguvu utayari wake wa kushiriki katika siku hiyo kubwa.

Katika muktadha huo, katika miji ya Samahij, Sitra na Jannusan, kuta za miji hiyo ziliandikwa kaulimbiu za kimapinduzi na jumbe za kuonesha mshikamano na wafungwa wa kisiasa wanaoshikiliwa katika magereza ya utawala wa Aal Khalifa.

Vilevile, bango kubwa lenye picha za mashahidi wa mji wa Al-Nuwaidrat liliwekwa katika njia ambayo msafara wa waombolezaji ulipita. Aidha, jina la mtawala dhalimu Hamad bin Isa Aal Khalifa liliandikwa kwenye barabara za mji wa Al-Markh, ili kuendeleza maandamano na matendo ya kuupinga utawala huo kwa njia mbalimbali.

Maandamano ya Maombolezo ya Kifo cha Kishahidi cha Bibi Fatima Zahra (sa) Chini ya Vitisho vya Usalama

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha