Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, ziara hiyo ambayo imekuwa ni fursa muhimu katika kuimarisha uhusiano wa kielimu na kidini, pamoja na kukuza mawasiliano na kubadilishana uzoefu baina ya wanazuoni na taasisi za Hawza zinazojihusisha na elimu ya dini ya Kiislamu.
Katika ziara hiyo, wanazuoni hao mashuhuri kutoka Najaf Al-Ashraf walipata fursa ya kukutana na Sheikh Jalala pamoja na jopo la uongozi wa Hawza ya Imam Swa'diq (a.s) katika ofisi yake. Katika mazungumzo yao, pande hizo zilipata nafasi ya kubadilishana fikra na uzoefu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusiana na elimu ya Hawza na shughuli za kidini.
Aidha, ziara hiyo imebeba ujumbe wa kuendeleza mshikamano na ushirikiano baina ya wanazuoni, hususan katika juhudi za kuimarisha elimu ya Kiislamu, kukuza mahusiano baina ya Hawza na kuendeleza mawasiliano kati ya vituo vya elimu ya dini vilivyopo katika maeneo mbalimbali ya dunia.
Baada ya mazungumzo hayo, wageni hao pamoja na Sheikh Jalala na jopo lake walipiga picha ya pamoja nje ya Msikiti wa Masjid Ghadiir, uliopo Kigogo Post, jijini Dar es Salaam.
Ziara hii ni miongoni mwa fursa zinazochangia kuimarisha mahusiano baina ya wanazuoni na taasisi za elimu ya dini, huku ikifungua milango ya kubadilishana maarifa na uzoefu kwa manufaa ya maendeleo ya elimu ya Kiislamu na jamii kwa ujumla.




Maoni yako