Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza A‘rafi, Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran, katika ujumbe wake alimpongeza Hujjatul-Islam wal-Muslimin Muhammad Hasan Jamshidi, pamoja na wasimamizi na wahudumu wote wa mawakibu, kwa juhudi zao za kuandaa na kuendesha maukibu, pamoja na ubunifu, mipango na shughuli mbalimbali zinazofanyika katika maukibu hiyo.
Katika ujumbe huo, huku akizungumzia nafasi ya wanazuoni wa Hawza katika hali ya sasa ya nchi, amesema: “Katika hali hii nyeti, nafasi ya ‘Hawza inayoongoza na iliyo mstari wa mbele’, pamoja na wanafunzi na walimu vijana, sambamba na wananchi na vijana wengine, ni nzito sana na ya kimkakati. Wajibu wao ni kujibu mahitaji ya kiakili, kimaarifa, kihisia na kiroho ya zama hizi mpya, kwa kuzingatia mabadiliko yanayoendelea sasa; kutoa mwongozo na kushiriki kikamilifu katika vita hivi vya sasa visivyo na usawa na vya mseto; kutoa ufafanuzi sahihi na kusimulia matukio kwa usahihi; kuchochea ari, kutoa uelewa, kujenga mshikamano, kutoa maarifa, kuimarisha utambuzi na uelewa wa mambo, pamoja na kufanya jihadi ya kielimu, kiutendaji na ya kimahubiri. Ni lazima kuweka matumaini katika rasilimali hizi zilizopo hivi sasa za taifa, vijana na Hawza.”
Ujumbe kamili wa Ayatullah A‘rafi ni kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
MheshimiwaHujjatul-Islam wal-Muslimin, Bwana Muhammad Hasan Jamshidi (Mwenyezi Mungu azidi kukuwezesha kufanikiwa),
Pamoja na wasimamizi na wahudumu wote wapendwa wa mawakibu,
Amani na salamu ziwe juu yenu. Nawaombea mafanikio zaidi.
Ninaona kuwa ni wajibu wangu, kwa niaba ya Hawza, kutoa shukrani na pongezi zangu za dhati kwako pamoja na washiriki wote wanaojitolea katika mawakibu, hususan mawakibu za “Istighatha” zilizopo Qum na katika Madrasatul-Hadhrat Sayyid al-Shuhada (as). Ninathamini na kusifu ubunifu, mipango na shughuli za maukibu hiyo tukufu, pamoja na juhudi za washiriki wake na vijana wetu wapendwa, na ninatoa heshima na shukrani zangu kwao.
Ukweli ni kwamba, kutokana na vita vya Ramadhani vilivyolazimishwa dhidi yetu, ukurasa mpya umefunguliwa katika historia ya Uislamu, Iran na Mapinduzi ya Kiislamu. Hatua mpya ya maendeleo katika mchakato wa Mapinduzi ya Kiislamu na katika zama za Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu ainue daraja lake) imeanza, kuelekea katika malengo ya kimataifa na ya kistaarabu ya Mapinduzi ya Kiislamu.
Kwa baraka za mawimbi yaliyoibuka kutokana na damu safi za mashahidi mashujaa wa Uislamu na Iran, pamoja na mashahidi wa mhimili wa Muqawama, na hususan damu takatifu ya kiongozi, mkuu na Imam shahidi, Ayatullah Khamenei (Mwenyezi Mungu amrehemu), kumeibuka mwamko wa kipekee miongoni mwa taifa na vijana.
Sambamba na ushujaa, ujasiri na kung’ara majeshi ya ulinzi na mhimili wa Muqawama, pamoja na juhudi za viongozi wanaotekeleza majukumu yao kwa ari ya jihadi, enzi mpya imeanza na mizania nyingi ya kikanda na kimataifa imebadilika kwa kiasi kikubwa.
Kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, na kwa juhudi na azma kubwa ya taifa la Iran, mhimili wa Muqawama na Umma wa Kiislamu, chini ya uongozi na mwongozo wa Kiongozi Mkuu (Mwenyezi Mungu aendelee kumhifadhi), pamoja na maelekezo ya Marajii wakuu wa kidini na jihadi ya majeshi yetu pendwa ya ulinzi, harakati hii ya kasi itaendelea kusonga mbele. Dhoruba hii ya Mwenyezi Mungu itazifutilia mbali njama na mipango ya maadui wenye chuki na wasio na huruma, adui wa Marekani na Uzayuni, pamoja na vibaraka wao.
Katika mazingira haya, nafasi ya “Hawza inayoongoza na iliyo mstari wa mbele”, pamoja na wanafunzi na walimu vijana, sambamba na wananchi na vijana, ni nzito sana na ya kimkakati. Wajibu wao ni kujibu mahitaji ya kiakili, kimaarifa, kihisia na kiroho ya zama hizi mpya, kwa kuzingatia mabadiliko ya sasa; kutoa mwongozo na kushiriki kikamilifu katika vita hivi vya sasa visivyo na usawa na vya mseto; kutoa ufafanuzi sahihi na kusimulia matukio kwa usahihi; kuchochea ari, kutoa uelewa, kujenga mshikamano, kutoa maarifa, kuimarisha utambuzi na uelewa wa mambo, pamoja na kufanya jihadi ya kielimu, kiutendaji na ya kimahubiri.
Kwa hiyo, ni lazima kuweka matumaini katika rasilimali hizi zilizopo hivi sasa za taifa, vijana na Hawza za kielimu.
Tafadhali zifikisheni salamu zangu na shukrani zangu kwa marafiki na ndugu wote.
Shukrani zisizo na kikomo.
Alireza A‘rafi
Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran
Maoni yako