Jumatano 30 Septemba 2026 - 08:02
Barua ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran, Kuwaelekea Wananchi wa Marekani

Barua ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa wananchi wa Marekani, ambayo imetolewa na msemaji wa jeshi hilo jana asubuhi katika mkutano na waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, maandishi ya barua ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa wananchi wa Marekani, ambayo mkutano wa kuielezea wa waandishi wa habari ulifanywa na msemaji wa Jeshi hilo, imechapishwa. Maandishi ya barua hiyo ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

««إِنَّ اللَّهَ لَا یُغَیِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّیٰ یُغَیِّرُوا مَا 
بِأَنفُسِهِمْ»

(Qur’ani Tukufu, 13:11)»

Wananchi waheshimiwa wa Marekani, wanasayansi, wanafunzi wa vyuo vikuu na wanahabari,

Kwa heshima na salamu za shukrani zizielekee roho za Mitume watukufu, hususan Nuhu, Ibrahim, Musa, Isa na Muhammad, rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao.

Miezi saba iliyopita, jeshi vamizi la Marekani, kwa kukiuka sheria za kimataifa, lilianzisha vita dhidi ya Iran kupitia uhalifu wa kivita kwa kushambulia shule ya msingi ya Minab na kuwaua watoto wanafunzi 168, na wakati huohuo kushambulia ofisi ya Imam Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, na kumuua yeye pamoja na familia yake, akiwemo mjukuu wake mwenye umri wa miezi 14. Katika vita hivyo, hadi sasa zaidi ya watu 3,600, ambao wengi wao walikuwa raia, wakiwemo watoto 400, wameuawa, huku vyuo vikuu 8, hospitali 3 na shule 8 zikilipuliwa. Hata hivyo, licha ya vitendo vya kiharamu na uhalifu usio na mfano katika vita hivi, Marekani na Israel walishindwa vibaya, na Mapinduzi ya Kiislamu yakapata ushindi mkubwa.

Sababu za ushindi wa Iran katika kukabiliana na mashambulizi ya Marekani

Kwa nini Iran ilishinda vita ikiwa na bajeti ya kila mwaka ya ulinzi inayolingana na asilimia moja tu ya bajeti ya ulinzi ya Marekani?

Ili kumtambua mshindi wa vita, ni lazima kuangalia ni upande gani ulifikia malengo yake. Viongozi na taasisi za Marekani na Israel hapo awali zilisema kwamba lengo la kuishambulia Iran lilikuwa “kubadilisha mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu” na “kuigawa Iran.” Lakini baada ya kushindwa katika malengo hayo mawili, katika vita visivyokuwa na mkakati, kila wiki walikuwa wakitoa lengo jipya:

“Iran ijisalimishe bila masharti yoyote,” “kuteka Kisiwa cha Khark na kutawala mafuta ya Iran,” “kufanya mashambulizi ya ardhini na kuteka ardhi ya Iran,” “kuangamiza miundombinu yote ya viwanda,” “kuangamiza miundombinu yote ya nishati na kuirejesha Iran katika zama za mawe,” “kuangamiza ustaarabu wa Iran,” “kufanya operesheni ya uhuru na kuudhibiti Mlango-Bahari wa Hormuz,” “kuzuia mauzo ya nje na uagizaji wa bidhaa kwenda Iran,” “kuangamiza sekta ya nyuklia,” “kuangamiza uwezo wa makombora na ndege zisizo na rubani,” “kuufanya Mlango-Bahari wa Hormuz kuwa sehemu ya ardhi ya Marekani na kutoza ushuru wa asilimia 20,” “kuangamiza mfumo wa ulinzi wa anga na kuitawala anga ya Iran,” na “kukomesha uungaji mkono wa Iran kwa Muqawama wa Kiislamu.”

Hayo yalikuwa malengo mapya 13 ambayo Rais wa Marekani aliyataja baada ya kushindwa katika malengo mawili ya awali wakati wa vita.

Mifano halisi ya ushindi wa Jamhuri ya Kiislamu

Ushindi wa Iran haukuishia tu katika kumzuia adui kufikia malengo yake. Ushindi mkubwa ulikuwa kwamba nguvu na hadhi ya jeshi la Marekani vilivunjwa, na katika vita hivi Marekani ilishushwa kutoka nafasi yake ya kuwa dola yenye nguvu kubwa duniani. Ushindi huu mkubwa kwetu ulikuwa kushindwa kusikoweza kurekebishwa kwa mfumo wa ubeberu.

Zaidi ya ndege zisizo na rubani 200 za kimkakati na za gharama kubwa, ndege 12 za kujaza mafuta na usafirishaji, ndege 30 za kivita, takriban ndege moja ya AWACS, makumi ya helikopta, makumi ya mifumo ya rada na ulinzi wa anga yenye gharama kubwa sana, pamoja na zaidi ya vitengo 350 vya vituo na miundombinu ya vituo vya kijeshi vya Marekani, viliharibiwa. Uwezo wa kiutendaji wa vituo 18 vya kijeshi vya Marekani katika eneo hilo ulifikishwa karibu na sifuri.

Sababu kuu ya kushindwa Marekani na Israel

Lakini sababu kuu ya kushindwa Marekani, licha ya kuwa na wingi wa silaha, si tu ukosefu wa uongozi unaostahili. Bali ukipima uongozi mkuu wa majeshi ya Marekani kwa vigezo vile vile ambavyo uongozi nchini Iran hupimwa—yaani, kwa vigezo vya elimu na utaalamu, hekima, ukweli, usafi na uchamungu, ujasiri na uelewa wa wakati—utakubali kwamba kwa namna ya kushangaza na isiyoaminika, umechaguliwa kwa asilimia mia moja kinyume kabisa na viashiria hivi sahihi vya ustahiki.

Je, Wairani wana uadui na wananchi wa Marekani? Ikiwa si hivyo, kwa nini wanatoa kauli ya “Mauti kwa Marekani”? Na uhusiano wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi na ugaidi ni upi?

Maumivu ya pamoja ya mataifa ya Iran na Marekani

Taifa la Iran na taifa la Marekani, kila moja kwa namna yake, limekumbwa na dhuluma za watawala wa Ikulu ya White House. Chanzo cha maumivu yetu ya pamoja ni kwamba watawala madikteta wa White House, ambao hukusanya kura za wananchi kupitia propaganda za kupotosha, si wawakilishi halisi wa wananchi wa Marekani, bali ni wawakilishi wa matajiri wakubwa wa Kizayuni. Na ili kupata ridhaa yao, hawakiuki tu haki za mataifa mengine, bali pia wanavunja haki zenu, na daima hutanguliza maslahi ya Wazayuni mbele ya maslahi ya wananchi wa Marekani.

Dhuluma ambayo viongozi wa White House wanawafanyia wananchi wa Marekani si ndogo kuliko dhuluma wanayowafanyia mataifa mengine; huenda hata ikawa ni kubwa zaidi. Ili kuelewa ukweli huu, kuna dalili nyingi.

Maana ya “Mauti kwa Marekani”

Kwa hiyo, maana ya kauli “Mauti kwa Marekani” haiwezi kuwa ni mauti kwa wananchi wa Marekani, ambao wenyewe wamekuwa waathirika wa dhuluma. “Mauti kwa Marekani” ni mauti kwa watawala madhalimu wa White House; ni kilio kinachotokana na maumivu ya dhuluma. Je, hata jambo hili linapaswa kunyimwa mwenye kudhulumiwa?

Uhusiano wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi na ugaidi

Kama kawaida, mfumo wa utawala wa mabavu hucheza na dhana kwa namna unavyotaka, huzibadilisha kulingana na maslahi yake, na hutumia uwezo wake wote kuzifanya zikubalike. Ugaidi na haki za binadamu ni mifano ya dhana ambazo zimechezewa na kubadilishwa maana.

Miongoni mwa michezo ya kushangaza zaidi katika siasa ni kwamba waathirika waliodhulumiwa zaidi na ugaidi wa kikatili wanatuhumiwa kuwa magaidi, tena na watu ambao wenyewe wana nafasi kuu katika kuwaandaa na kuwahamasisha magaidi. Wale wanaoinuka dhidi ya dhuluma na uvamizi huitwa magaidi, na mara tu wanapojisalimisha na kushiriki katika uhalifu wa wavamizi, huondolewa katika orodha ya magaidi. Hakuna kigezo kingine katika suala hili isipokuwa kutekeleza maslahi ya Uzayuni.

Kwa nini serikali ya Marekani inaelekea kuanguka

Ukatili, kupindukia katika dhuluma na umwagaji damu, kuenea uwongo, kuwapa watu duni nafasi ya mbele kuliko watu wenye fadhila na wanasayansi, kujishughulisha na masuala ya pembeni na kupuuza masuala ya msingi, ni miongoni mwa mambo ambayo wenye hekima mashuhuri katika historia wameyachukulia kuwa ni alama za mwisho na kudhoofika kwa tawala. Na sifa zote hizi zinaakisi hali ya utawala wa Marekani leo.

Historia ya uvamizi na ukatili wa Marekani duniani

Si Iran pekee iliyokuwa katika hatari ya kukumbwa na uhalifu wa kutisha wa serikali ya Marekani. Tangia katikati ya karne ya 20, wakati Marekani ilipojitokeza kama dola yenye nguvu kubwa duniani, takriban nchi 70 zimevamiwa kijeshi au zimekumbwa na mapinduzi ya kijeshi na uingiliaji wa moja kwa moja wa hujuma uliofanywa na Marekani.

Wananchi wa nchi mbalimbali duniani, kama vile Japan, Korea, Vietnam, Cambodia, Ufilipino, Libya, Sudan, Afghanistan, Iraq na Syria, wamepitia mauaji ya halaiki yaliyowaua mamia ya maelfu ya watu na wakati mwingine mauaji ya kimbari yaliyowaua mamilioni ya watu yaliyofanywa na Marekani. Na nchi nyingine nyingi kama vile Cuba, Mexico, Nicaragua, Venezuela, Panama, Chile, Brazil, Lebanon na Palestina na nyinginezo, zina majeraha makubwa yaliyosababishwa na utawala wa Marekani.

Uongo, msingi wa utawala wa Marekani

Maamuzi muhimu zaidi ya White House yenye kuamua hatima hujengwa juu ya uongo. Huko, uwongo hauna mwisho; ni uwongo ambao kila mmoja wao umesababisha janga duniani. Hawajali kuaibishwa na uwongo huu; uwongo kuhusu nafasi ya Afghanistan katika shambulio la minara miwili pacha, uwongo kuhusu kuwepo silaha zisizo za kawaida nchini Iraq, na kadhalika. Na uwongo wa karne ni madai kwamba Iran ina bomu la nyuklia, jambo ambalo hata mtu mjinga anaweza kutambua kwamba ni uongo.

Kuwatanguliza watu duni mbele ya watu wenye fadhila na wanasayansi

Kuwekwa viongozi wasio na busara na hekima katika uongozi wa nchi, ambao huona tu kile kilicho mbele ya pua zao na bila kuwa na mtazamo wa mbali wala kuangalia mustakabali, hufuata malengo na mipango mibaya ambayo ili kurekebisha madhara yake hulazimika kutumia gharama mara kadhaa zaidi, na huanzisha “mizunguko mibovu” ambayo kama kimbunga huivuta nchi yenu ndani yake.

Kujishughulisha na masuala ya pembeni na kupuuza masuala ya msingi

Rais wa Marekani anaifanya nchi ishughulike na mambo ya pembeni kama vile ukumbi wa dansi wa White House, kubadilisha jina la Ziwa Ontario na Ghuba ya Mexico, kupaka rangi bwawa la kuakisi, na kuweka jina lake kwenye mabango ya Kituo cha Kennedy, huku masuala ya msingi kama kudhibiti mfumuko wa bei unaoongezeka, afya ya Wamarekani, gharama za makazi na mengineyo yakiachwa bila kushughulikiwa.

Vita hivi vitafikia wapi?

Kiongozi wetu aliyefariki shahidi alikuwa ameshaonya kwamba ikiwa adui atashambulia, vita vitakuwa vya kikanda. White House haikuamini, ikashangazwa na hali hiyo na kufikia mwisho wa njia.

Alisema: “Ikiwa jambo lolote litatokea, taifa la Iran litafufuliwa na litamaliza kazi.”

Utabiri huo pia umetimia, na mamilioni ya Wairani kwa muda wa miezi saba sasa wamekuwa mitaani kila usiku wakitaka kulipiza damu ya Imam wao aliyefariki kishahidi.

Kwa matumaini ya kukomeshwa dhuluma na uvamizi wote, ukombozi wa mataifa yote kutoka katika utumwa wa madhalimu, na kuishi katika undugu na amani ya dunia.

««وَلَقَدْ كَتَبْنَا فِي الزَّبُورِ مِن بَعْدِ الذِّكْرِ أَنَّ الْأَرْضَ يَرِثُهَا عِبَادِيَ الصَّالِحُونَ»

(Qur’ani Tukufu, 21:105)»

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha