Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Shule hiyo inayojikita katika kutoa elimu ya kawaida pamoja na elimu ya dini, imeendelea kuwa na dhamira ya kuhakikisha watoto wanapata malezi yanayowawezesha kukua kielimu, kiroho na kimaadili, huku wakijengewa misingi imara ya kumjua Mwenyezi Mungu, kuipenda dini na kushikamana na mafundisho ya Ahlul Bayt (a.s).
Katika hatua nyingine ya kuboresha huduma zake za kielimu na malezi, uongozi wa shule hiyo umetangaza kuwa, Inshaallah, kuanzia mwezi Januari mwakani kutaanzishwa huduma ya bweni kwa wanafunzi kuanzia darasa la kwanza. Hatua hiyo inalenga kutoa fursa zaidi kwa wazazi na walezi wanaotamani watoto wao kupata elimu bora sambamba na malezi ya kidini na kimaadili katika mazingira yanayozingatia misingi ya Kiislamu.
Akizungumza kuhusu dhamira ya shule hiyo, Mkurugenzi wa Shule hiyo Sheikh Abdulatif Swaleh, ameeleza kuwa; shule imejipanga kupokea watoto na kuwalea kwa mujibu wa mafundisho ya Ahlul Bayt (a.s), kwa kuzingatia malezi ya kiroho, mwenendo mwema na misingi sahihi ya kiimani, ili kuwajenga kuwa kizazi chenye elimu, maadili na uwajibikaji katika jamii.
Aidha, shule hiyo imetoa wito kwa wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao katika taasisi hiyo, ikiwahakikishia kuwa itashirikiana nao katika kuhakikisha watoto wanakua katika misingi ya Wilaya ya Ahlul Bayt (a.s), huku wakipata elimu itakayowasaidia katika maisha yao ya sasa na ya baadaye.
Mahafali hayo ya tatu yamefanyika chini ya usimamizi wa Mkurugenzi wa Lady Zahraa Islamic School, Sheikh Abdulatif Swaleh, ambaye pamoja na uongozi wa shule hiyo wanaendelea na juhudi za kuhakikisha taasisi hiyo inatimiza malengo yake ya kielimu na kimalezi.
Kwa mantiki hiyo, wazazi na walezi wote wanaotamani watoto wao wapate elimu inayounganisha maarifa ya kawaida, elimu ya dini na malezi yenye misingi ya Ahlul Bayt (a.s), wanakaribishwa kujiunga na Lady Zahraa Islamic School, Kondoa.
Lady Zahraa Islamic School – Mahali pa kujenga kizazi chenye elimu, imani na maadili mema.







Maoni yako