Alhamisi 1 Oktoba 2026 - 09:35
Kuifanya Swala kuwa sehemu ya msingi na jambo la watu wote katika jamii ni msingi wa kuifikia jamii ya Kiislamu/ Maimamu wa Jamaa na wa Swala ya Ijumaa wanapaswa kuwa mahali pa usalama kwa watu, sikio linalosikiliza na kupokea malalamiko na matatizo yao

Hawza/ Swala kufanywa kuwa sehemu ya msingi ya maisha, kuenea na kuwa jambo la watu wote katika jamii, na kisha kuwepo juhudi za pamoja za kuitekeleza kwa uzuri, ni pande mbili kuu za mchakato wa juhudi za kufikia lengo hili. Kuimarisha na kustawisha misikiti, pamoja na maandalizi mengine kwa ajili ya kuongeza idadi na kuboresha ubora wa Swala za Jamaa na Swala za Ijumaa, ni mambo ya msingi yanayohitajika ili kufikia lengo hili muhimu. Katika mambo yote haya, nafasi ya Maimamu wa Jamaa na Maimamu wa Swala ya Ijumaa, ambao wanapaswa kuwa mahali pa usalama kwa watu na kuwa sikio linalosikiliza na kupokea maumivu na matatizo yao, ni kubwa sana.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, maandishi ya ujumbe wa Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, kufuatia Mkutano wa 33 wa Kitaifa wa Swala ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Kuzingatia jambo tukufu la “kusimamisha Swala”, na hususan kuandaliwa Mkutano wa Swala, ni miongoni mwa hatua muhimu na zinazostahili kuchukuliwa ambazo, tangu mwanzoni mwa miaka ya sabini, zimeanzishwa nchini Irani, kwa juhudi za mwanazuoni mwenye juhudi na anayejitolea kwa ajili ya watu, mwalimu wa Qur’ani na mhubiri mahiri, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Qara’ati, Mwenyezi Mungu aendelee kumhifadhi.

Uangalizi maalumu uliotolewa na Kiongozi Mkuu wa thamani, Shahidi, Mwenyezi Mungu autukuze utukufu wa cheo chake, kwenye jambo hili, pamoja na nasaha zake muhimu, endelevu na zenye kusisitizwa katika jumbe zake zinazohusiana na mikutano 32 iliyopita, pia unaongeza umuhimu wa mwelekeo huu.

Bila shaka, kuzungumza au kuandika kuhusu Swala kunastahili kufanywa kwa kiwango na hadhi ya wahyi wa Mwenyezi Mungu na maneno ya Mtume Mtukufu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie yeye na Ahlu Bayt wake, pamoja na Maimamu Maasumin, amani na rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao. Na kalamu ya watu kama mimi ni ndogo mno kiasi cha kuweza kuandika jambo kuhusu kina cha maarifa ya Swala.

Hata hivyo, utambulisho na mahitaji ya jamii ya Kiislamu, pamoja na majukumu ya watumishi wake, hususan uongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, vinafanya iwe muhimu kwangu kujikumbusha mwenyewe, pamoja na watu wote na viongozi, mambo machache kwa mtazamo huu.

Swala ni miongoni mwa neema kubwa na nzuri zaidi za Mwenyezi Mungu Mtukufu, ni taasisi, nembo na nguzo kuu ya dini, na ni kamba ya kumunganisha kila mmoja wetu ili aweze kuwasiliana kwa karibu na moja kwa moja na chanzo kisicho na kikomo wala mwisho cha Mwenyezi Mungu.

Dawa hii ya mafanikio na uokovu, na nguzo ya maisha mema, ni tegemeo imara na endelevu, pamoja na akiba isiyokwisha ya mwanadamu katika mapambano dhidi ya shetani wa nafsi na mashetani wa kidunia. Aidha, ni chemchemi inayobubujika ya mapenzi, matumaini, huruma na utulivu. Na kushuka baraka na kuongezeka riziki za Mwenyezi Mungu hutokea na kuongezeka kupitia kusimamisha Swala na kuomba msamaha.

Hata hivyo, faradhi ya Swala si jukumu la mtu binafsi pekee. Kwa mujibu wa mafundisho ya Qur’ani, kusimamisha Swala ni tunda na alama ya kwanza ya utawala wa watu wema, kama inavyosema:

«اَلّذینَ اِنْ مَکَّنّاهُم فی الأرضِ اَقاموا الصَّلاة»

“Ambao tukiwapa uwezo na mamlaka katika ardhi, husimamisha Swala.”

Kuwekwa aya hii mara tu baada ya aya inayotoa ahadi ya msaada wa Mwenyezi Mungu kuhusu wafuasi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na jihadi yao katika Sura Tukufu ya Hajj, kunaonesha kwamba kusimamisha Swala, ikiwa ni tegemeo imara la kumdhukuru Mwenyezi Mungu, kuwa na matumaini kwake na kumtegemea, kuna nafasi maalumu katika jihadi, ushindi na kufanikiwa katika medani za mapambano, hususan medani ya mapambano ambayo leo iko mbele ya taifa la Iran.

Leo, ambapo masharti ya uwezo na nguvu ya wananchi wapendwa wa Iran yameandaliwa zaidi kuliko hapo awali, kila mmoja katika taifa hili lililopewa ujumbe, anakabiliwa na amri hii ya Mwenyezi Mungu ya kusimamisha Swala kila wakati:

«اَقیموا الصَّلاة»

“Simamisheni Swala.”

Zaidi ya hayo, watu wote wenye ushawishi katika jamii, kuanzia akina baba na akina mama na familia, hadi walimu na marafiki; kuanzia maprofesa na wasomi hadi watu wanaotambulika na watu mashuhuri; na vilevile taasisi na vyombo vyote vinavyounda utamaduni, miongoni mwao misikiti, Swala za Ijumaa, shule, vyuo vikuu, Hawza, Shirika la Redio na Televisheni, wanaharakati wa kitamaduni na kijamii, pamoja na Basij ya wananchi, hususan wale wanaowasiliana na tabaka la vijana balehe na vijana, wote wana jukumu la ziada katika jambo hili.

Kusimamisha Swala katika hatua zake zote za ukamilishaji na viwango vyake mbalimbali vya maendeleo ndani ya jamii na nchi ambayo imeinua bendera ya Uislamu safi wa Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie yeye na Ahlu Bayt wake, na imeheshimiwa kwa kuwa chini ya utawala wa Uislamu, ni miongoni mwa mambo muhimu zaidi. Na ili kuweka mazingira ya kupita katika njia kutoka hatua ya harakati na Mapinduzi ya Kiislamu hadi hatua ya jamii ya Kiislamu, jambo hili ni la lazima. Baada ya hapo ndipo kufikia hatua ya ustaarabu wa Kiislamu kutakapowezekana.

Kufanywa Swala kuwa sehemu ya msingi ya maisha, kuenea na kuwa jambo la wote katika jamii, na kisha kuwepo juhudi za pamoja za kuitekeleza kwa uzuri, ni pande mbili kuu za mchakato wa juhudi za kufikia lengo hili. Kuimarisha na kustawisha misikiti, pamoja na maandalizi mengine kwa ajili ya kuongeza idadi na kuboresha ubora wa Swala za Jamaa na Swala za Ijumaa, ni mambo ya msingi yanayohitajika ili kufikia lengo hili muhimu. Katika mambo yote haya, nafasi ya Maimamu wa Jamaa na Maimamu wa Swala ya Ijumaa, ambao wanapaswa kuwa mahali pa usalama kwa watu na kuwa sikio linalosikiliza na kupokea maumivu na matatizo yao, ni kubwa sana.

Ninatumaini kwamba kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na kwa mazingatio pamoja na dua maalumu ya Bwana wetu, Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake, watu na nchi yetu pendwa watafanikiwa na kusaidiwa katika jambo la kusimamisha Swala na kunufaika na fadhila na baraka zake.

Sayyid Mujtaba Husayni Khamenei

9 Mwhr 1404/ Oktoba 1 2026.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha