Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kutokana na maswali yaliyoulizwa kuhusu hukumu ya kisheria ya kununua na kuuza bidhaa na huduma zinazohusiana na utawala wa Kizayuni, fatwa za Maraji zinaonesha kwamba hatua yoyote ya kiuchumi inayosababisha kuimarishwa utawala huo si jambo linaloruhusiwa, na wenye wajibu wa kisheria wanapaswa kuliepuka.
Hujjatul-Islam Amini, mtaalamu wa hukumu za kisheria, anajibu kuhusu suala hili:
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
Katika mfululizo wa mijadala inayohusiana na kununua na kuuza bidhaa za nchi ambazo kwa sasa ziko vitani nasi (Iran), miongoni mwao ukiwa ni utawala bandia wa Kizayuni, nilikuwa nawasilisha baadhi ya mambo.
Jambo la pili ambalo katika kikao hiki ninawasilisha mbele ya ndugu wapendwa ni kwamba katika maswali ambayo kwa kawaida huulizwa, huuliza hivi:
Je, kununua na kuuza bidhaa, kama vile za Kizayuni kuna tatizo au hakuna tatizo?
Tulieleza kwamba Maraji wamesema jambo hili ni haramu; lakini kwa usahihi zaidi, haijalishi aina ya manufaa mnayoyatoa na ambayo yanafika kwa kampuni za Kizayuni ikiwa yanapatikana kupitia ununuzi na uuzaji. Inawezekana isiwe ni ununuzi na uuzaji, bali ni utoaji wa huduma na kampuni za Kizayuni.
Kwa mfano, tuchukulie kwamba mtu anatumia tovuti fulani katika anga ya mtandao, ambapo anapoingia katika tovuti hiyo, ili kutumia huduma zake anapaswa kulipa gharama fulani, au anatumia akili bandia ambayo sehemu ya faida inayopatikana kutokana na akili hiyo bandia inazisaidia serikali za Kizayuni, Hakuna tofauti. Kwa hiyo, ununuzi na uuzaji, kwa lugha yetu sisi wanafunzi wa Hawza, si jambo lenyewe linalozingatiwa; jambo muhimu ni aina yoyote ya kuimarisha.
Kwa hiyo, ikiwa mnaingia katika tovuti ambayo ili kutumia huduma zake mnahitaji kulipa kiasi fulani cha fedha, na mnajua kwamba fedha hizo zitaufikia utawala bandia wa Kizayuni, jambo hili pia lina tatizo.
Vilevile, kampuni za usambazaji; wakati mwingine bidhaa yenyewe si ya Kizayuni na hata si mali ya nchi ambayo tuna tatizo nayo, lakini kampuni ya usambazaji, yaani mpatanishi katika mauzo, yaani yule anayesambaza bidhaa hizo na kuchukua asilimia fulani ya faida kwa ajili yake, huenda ikawa ni kampuni inayohusiana na utawala bandia wa Kizayuni. Hili pia ndugu wapendwa wanapaswa kulizingatia. Si bidhaa yenyewe pekee inayozingatiwa; aina yoyote ya kuimarisha, [ina tatizo].
Ikiwa ndugu yetu anafanya kazi mahali ambapo, kwa mfano, ni wakala wa kampuni fulani, na kampuni hiyo kwa sababu yoyote ile, inatoa sehemu ya faida zake kwa kampuni za Kizayuni hili pia lina tatizo.
Kwa hiyo, jambo nililotaka kuwaeleza katika kikao hiki ni kwamba iwe ni ununuzi na uuzaji, au iwe kupitia kulipa gharama kwenye tovuti na kutumia huduma za tovuti hiyo, au mtu amewekeza katika baadhi ya masoko ya kifedha ambapo wakala wa kati anayeshughulikia shughuli hiyo ni wakala ambaye anapokea sehemu ya faida na kupeleka sehemu hiyo ya faida kwa kampuni za Kizayuni, au yeye mwenyewe ni Mzayuni.
Wewe unafanya shughuli katika soko la kifedha; kwa mfano, kununua na kuuza sarafu, kununua na kuuza euro, kununua na kuuza dola; lakini wakala ambaye unafanya naye kazi, ima moja kwa moja ni Mzayuni au anahusishwa na kampuni zinazolipa kodi katika nchi za Kizayuni, miongoni mwao ikiwa ni Israel.
Ndugu wapendwa wanapaswa kuzingatia kwamba aina zote za kuimarisha nchi kama vile utawala bandia wa Kizayuni, kwa mujibu wa hukumu ya kisheria, ni haramu na haziruhusiwi.
Inshaallah mfanikiwe.
Wassalaamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakaatuh.

Maoni yako