Kwa mujibu wa Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ghazi Hanina, Mkuu wa Bodi ya Wadhamini ya “Muungano wa Wanazuoni wa Kiislamu wa Lebanon”, wakati wa kushiriki katika hafla kuu na yenye hamasa kubwa ambayo Hizbullah iliiandaa kwa ajili ya kumbukumbu ya mwaka wa pili wa kuuawa kishahidi Sayyid Hassan Nasrullah, Sayyid Hashim Swafiyu al-Din na wenzao, iliyofanyika kando ya kaburi la Shahidi wa Umma katika kitongoji cha kusini mwa Beirut, alisisitiza kushikamana na ahadi ambayo wana wa Muqawama waliitoa kwa Sayyid Hassan Nasrullah, Shahidi wa Umma. Pia alibainisha kwamba; njia hii itaendelea hadi Palestina ikombolewe na wavamizi “Waisraeli” waondolewe.
Sheikh Hanina amesema: Waliohudhuria, licha ya maumivu, huzuni na masikitiko yanayozikandamiza nyoyo, wanaiheshimu kumbukumbu na utajo wa Sayyid Nasrullah.
Ameongeza: Tutaendelea kubaki katika ahadi ileile ambayo ulitufungia, na katika ahadi ileile uliyotuahidi; hadi ukombozi wa Palestina, Palestina yote, na kuwaondoa maadui wa Kizayuni kutoka kusini yetu takatifu kutakapotekelezwa.
Sheikh Hanina, huku akirejea kwamba Sayyid Hassan Nasrullah alipanda matumaini na imani ndani yetu, amesisitiza: Njia hii na mtazamo huu vitaendelea.
Maoni yako