Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Ali al-Khatib, Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Mashia Lebanon, siku ya Jumatatu, katika makao makuu ya baraza hilo huko Hazmieh, aliupokea ujumbe wa Hawza za Iran ulioongozwa na Hujjatul-Islam Sayyid Mufid Husaini Kuhsari; ujumbe ambao ulikuwa umehudhuria kwa ajili ya kushiriki katika kumbukumbu ya mwaka wa pili wa kuuawa kishahidi Sayyid Hassan Nasrullah, Sayyid Hashim Safi al-Din na viongozi wakuu wa Muqawama.
Katika mkutano huo, yalijadiliwa maendeleo ya hali ya Lebanon na eneo hili katika kivuli cha mashambulizi ya Marekani na Uzayuni.
Hujjatul-Islam Husaini Kuhsari, mwanzoni mwa mkutano huo, alitoa salamu za pole kwa mnasaba wa kuuwawa kishahidi mashahidi hao na kusema: Tunathamini msimamo wa watu wa Lebanon na Muqawama; ujumbe huu umekuja kushiriki katika hafla hii ya kumbukumbu ya mwaka na kufanya mikutano kwa ajili ya kuimarisha uhusiano na Hawza za Kiislamu.
Akirejelea msimamo wa Mashia nchini Lebanon na urithi wao mrefu, kuanzia Jabal Amil hadi Imam Musa Sadr, alieleza matumaini kwamba mhimili wa Muqawama na mataifa yake utabaki kuwa jambo thabiti katika harakati za uamsho.
Baada ya hapo, Sheikh al-Khatib katika hotuba yake alisema: Salamu za pole ni za pamoja. Tunajivunia kuwa katika njia hii; njia ambayo yeyote anayopiga hatua ndani yake si mwenye kushindwa, kwa sababu ni njia ya haki na uokovu, hii ndiyo njia ya Manabii na Maimamu. Kwa hiyo, tunayaona mauaji ya kishahidi ya Sayyid Nasrullah na wenzake, pamoja na kuuawa kishahidi Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Shahidi Imam Sayyid Ali Khamenei, na mashahidi wengine, kuwa ni funzo katika njia hii, na katika matukio haya hatukuona chochote isipokuwa uzuri, kama ambavyo Bibi Zainab (sa) alisema mbele ya Yazid, tunahisi maumivu na mateso makali, lakini hatuoni jambo hili kuwa hasara.
Aliongeza: Kinachoendelea leo, mipaka yake haijulikani, lakini yeyote anayevuka bahari ataamini kwamba baada ya kuvuka itapatikana faraja na ufunguzi, nasi tuna yakini kwamba tutafika mahali tunapopaswa kufika. Hali ni ngumu na maumivu ni makali sana, lakini kama mnavyoona, watu wanavumilia maumivu haya, na maadamu juhudi zetu ziko katika njia iliyo sahihi, tunamuomba Mwenyezi Mungu asiipoteze juhudi hii.
Sheikh al-Khatib, akirejelea msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukabiliana na nguvu kubwa zaidi katika historia, ambayo ina utajiri na uchumi mikononi mwake, lakini ilishindwa mbele ya Jamhuri ya Kiislamu na ikabaki bila uwezo wa kuufungua Mlango-Bahari wa Hormuz, alibainisha: Leo dunia jambo lake kuu ni Iran na Mashia, wakati hakuna mtu aliyedhani kwamba Iran ingeweza kusimama dhidi ya nguvu hii kubwa.
Aliongeza: Israel si chochote isipokuwa kituo cha kivita cha Marekani. Maadamu lengo letu ni Mwenyezi Mungu na maadamu tuko upande wa haki, hatutaogopa, nina matumaini, na siku itafika ambapo tutasema: Ndiyo, msumeno umeishinda nyundo; kama ilivyotokea mwaka 2000.
Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Mashia pia alirejelea hali ya watu waliokimbia makazi yao, ambao nyumba zao zimebomolewa na makaburi ya wapendwa wao yamefukuliwa, na kusema: Kwa hakika, hatuko katika hali ya kuwa na nchi inayoweza kuwaokoa watu hawa kutokana na mateso yao, lakini sisi hatuangalii kwa mtazamo finyu wa kimadhehebu, bali tunawaangalia wengine kwa mtazamo wa kitaifa. Serikali imewaacha watu wake ambao wako katika uhitaji mkubwa, na sisi tunapaswa kutumia juhudi zetu zote na kushirikiana pamoja ili kuwatoa watu katika mateso haya.
Maoni yako