Alhamisi 26 Novemba 2026 - 13:30
Wanazuoni wa Lebanon watafanya mkutano wa dharura

Hawza/ Hawza, mikusanyiko na taasisi za kidini nchini Lebanon zimetangaza kufanyika mkutano wa wanazuoni kwa lengo la kutangaza mshikamano na masuala yanayowahusu wanazuoni wa Bahrain na kulaani hukumu za dhuluma za kifungo cha maisha zilizotolewa dhidi yao. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi, tarehe 26 Novemba 2026 (5 Azar 1405), mjini Beirut.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hawza za kielimu, mikusanyiko pamoja na taasisi za kidini na za wanazuoni nchini Lebanon zimeitisha kufanyika mkutano wa wanazuoni kwa lengo la kutangaza mshikamano na masuala yanayowahusu wanazuoni wa Bahrain na kulaani hukumu za dhuluma zilizosababisha kutolewa kwa adhabu za kifungo cha maisha dhidi yao.

Mkutano huo utafanyika siku ya Alhamisi, tarehe 26 Novemba 2026 (5 Azar 1405), katika ukumbi wa “Al-Jinan”, uliopo kwenye barabara ya kuelekea uwanja wa ndege, eneo la Dahiyah Kusini mwa Beirut.

Wito huo umetolewa kufuatia wimbi kubwa la kulaani kutoka katika nchi za Kiarabu na Kiislamu dhidi ya hukumu zisizo za haki zilizotolewa na mahakama za utawala wa Aal Khalifa. Hukumu hizo zimetolewa dhidi ya zaidi ya wanazuoni 60 wa Kishia, ambapo baadhi yao wamehukumiwa kifungo cha maisha jela.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha